Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM

Shekau athibitisha mamlaka yake kwa Boko Haram

Kiongozi maarufu wa kuni la Boko Haram, Abubakar Shekau, ameahidi kuimarisha mapambano yake ya kijihadi katika tangazo alilolitoa katika video Jumapili usiku, huku akisema kuwa hakuna mgawanyiko wa ndani katika kundi hilo, habari iliyotolewa wiki iliyopita.

Picha ya Boko Haram iliyonaswa kwa video tarehe Agosti 7, kwenye mtandao, ambapo kiongozi wa kundi la wanajihadi Abubakar Shekau akionekana (katikati).
Picha ya Boko Haram iliyonaswa kwa video tarehe Agosti 7, kwenye mtandao, ambapo kiongozi wa kundi la wanajihadi Abubakar Shekau akionekana (katikati). HO / BOKO HARAM AFP / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mimi, Abubakar Ash-Shakawy (Shekau), kiongozi wa Jama'atu Ahlissunnah Lidda'awati Wal Jihad (jina la Boko Haram toka lijiunge nakundi la islamic State mwezi Machi 2015), napambana vita dhidi ya Nigeria na dhidi ya ulimwengu mzima, ikiwa ni wajibu wangu kibinafsi, "amesema katika video hiyo iliyorushwa kwenye mtandao wa YouTube, kisha ikafutwa, ambapo anaonekana, mwenye afya nzuri, huku akiwa amezungukwa na wapiganaji wawili wenye silaha.
kiongozi msimamo mkali

"Sina hamu ya kuua ndugu zetu Waislamu," ameongeza katika mkanda huo wa dakika 24, huku akipinga kukosolewa mara kwa mara na baadhi ya wanachama wa IS, ambao wanamuona Shekau kama kiongozi mwenye msimamo mkali, ambaye aliua maelfu ya watu tangu mwaka 2009, hasa Waislamu wengi.

Video hii ni jibu jipya kwa mahojiano ya Abu Mosab al-Barnawi na gazeti la kila wiki la kundi la IS la Al Nabaa, ambapo mtu huyo alionyeshwa Jumanne wiki iliyopita kama wali (kiongozi) mpya wa katika Afrika ya Magharibi. TAngu Alhamisi juma lililopita, Abubakar Shekau amekua akirusha hewani sauti zilizorekodiwa akithibitisha kwambabado "yupo" na hatomkubali "mjumbe yeyote" wa kundi la Islamic State.

Akibebelea silaha,huku akiwa ni mwenye furaha kuliko siku za nyuma, Shekau amethibitisha kwamba hajafariki au kupoteza nguvu za kupambana, kinyume na kile alichokizungumza katika video ya mwezi Machi ambapo alidai "kwangu mimi, nimefika mwisho. "

Msitu wa Sambisa

Katika hotuba yake, inayoonekana kuwa aliitolea katika msitu Sambisa ngome kuu ya kundi hilo kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa wataalam, Shekau anataka kuipa nafasi Boko Haram katika jihadi ya kimataifa, akizungumzia moja kwa moja Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.