Pata taarifa kuu
AU-RWANDA-DLAMINI ZUMA

Mkutano wa AU: Masuala nyeti yatakayozungumziwa Kigali

Mjini Kigali nchini Rwanda, sherehe ya ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) imefanyika Jumapili hii Julai 17. Wakuu wa nchi za Afrika wamekutana awali katika faragha kujadili mgogoro wa Sudan Kusini, lakini pia mrithi wa Nkosazana Dlamini-Zuma katika nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya AU na uwezekano wa Morocco kurejea kuwa mwanachama wa Umoja huo.

Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) unafunguliwa mjini Kigali, ambako mapigano ya hivi karibuni Sudan Kusini na mrithi Rais wa Tume ya AU vitatawala mkutano huu.
Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) unafunguliwa mjini Kigali, ambako mapigano ya hivi karibuni Sudan Kusini na mrithi Rais wa Tume ya AU vitatawala mkutano huu. © AFP/CYRIL NDEGEYA
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa kilele ulianza na kikao cha faragha kuhusu hasa hali inayojiri Sudan Kusini ambayo inawatia wasiwasi wakuu wa nchi wanaoshiriki mkutano huo tangu Jumapili asubuhi. Wakuu hawa wa nchi za Afrika, kwa kweli, wanahisi kwamba iwapo wataweka shinikizo kwa pande mbili, Salva Kiir na Riek Machar, viongozi hawa wanaweza kusimamisha machafuko ambayo yanaongezeka kila kukicha nchini Sudan Kusini.

Upi mpango wao ? Naam, Jumamosi usiku, Marais na viongozi wa serikali kadhaa walikutana katika hoteli kubwa ya kifahari mjini Kigali. Kulikuwepo Marais na viongozi wa serikali za Afrika Mashariki - ikiwa ni pamoja na Rais wa Sudan Omar al Bashir - Idriss Deby wa Chad, Paul Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Ramtane Lamamra wa Algeria na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Mpango wao unahusu uimarishaji wa vikosi vya Umoja wa Matifa (UNMIS)vya askari 12,000 waliotumwa nchini Sudan Kusini. Uimarishaji wa UNMIS utafanyika kupitia majukumu mapya ambayo watakapewa askari wa kulinda amani wa kuingilia kati baina ya pande zinazopigana nchini Sudan Kusini na piakwa ushirikiano na kikosi cha Umoja wa Afrika. Itakua ni kikosi cha askari wakutoka nchi za Afrika ambao wataingizwa katika UNMIS chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa.

Huu ni mpango wa Ban Ki-moon. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anafanya hivyo, kwa kuwa yuko mbioni kukamilisha kipindi chake - kabla ya Krismasi - juu ya kurudi kwa amani nchini Sudan Kusini na ni mpango ambao unaungwa mkono na Wakuu wote wa Ukanda na bara nzima.

Kinachosalia ni kuwashawishi wahusika, Salva Kiir na Riek Machar. Kwa sababu za wazi za kiusalama, wawili hao wameamua kusalia mjini Juba lakini labda watakuja mjini Kigali kila umoja upande wake. Hayo ni matakwa ya viongozi wa Afrika walioelezea Jumamosi usiku walipokutana. Walimuomba Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Idriss Déby, kujaribu kuwashawishi waje angalau masaa machache mjini Kigali hadi Jumatatu jioni.

Suala la mtu atakayemrithi Rais wa Tume ya AU bado ni mtihani

Wagombea watatu wa ndio wanawania nafasi ya Nkosazana Dlamini-Zuma anaye maliza muda wake kwenye Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU). Wagombea hao no pamoja na Mawaaziri wa Mambo ya Nje wa Botswana na Equatorial Guinea na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Uganda Speciosa Wandira-Kazibwe.

Tatizo? Wagombea hao hawatoshelezi vigezo vinavyotakiwa na nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS). ECOWAS imeomba uchaguzi huo uahirishwe ili kuwapa nafasi wagombea wengine. Hoja ambayo ambayo imewaudhi wafuasi wa kambi inayotaka uchaguzi huo ufanyike, na hivyo kusababisha mvutano.

Wagombea wengine ambao wamejulikana na huenda wakaruhusiwa kuwania ikiwa watapewa nafaasi ya kuwania katika kinyang'anyiro hiki. Wagombea hao ni pamoja na Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekuwa rais wa Tanzania, Profesa Abdoulaye Bathily anayewakilisha Umoja wa Mataifa katika Afrika ya Kati, ambaye ni raia wa Senegal na ambaye alikuwa na wakati wa kufanya na kuandaa kwa umakini kampeni zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.