Pata taarifa kuu
UA-BURUNDI-MASHAURIANO

UA-Burundi: upinzani wakata tamaa baada ya siku ya kwanza ya mashauriano

Alhamisi hii ilikua siku ya kwanza ya mazungumzo nchini Burundi kwa Ujumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma (kushoto) akipokelewa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kulia), Februari 25, 2016.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma (kushoto) akipokelewa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kulia), Februari 25, 2016. © STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo unaoundwa na viongozi wa tano kutoka nchi za Afrika, utajaribu kuendesha mashauriano ili kushawishi haja ya mazungumzo yatakayowashirikisha wadau wote wa taifa hilo nje ya Burundi kwa kujaribu kumaliza mgogoro unaoikumba nchi hiyo.

Ujumbe huo unatazamiwa kukutana kwa mazungumzo na Rais Nkurunziza, mkutano ambao ulikua umepangwa kufanyika Alhamisi hii jioni, haukufanyika kutokana na kuchelewa kwa ratiba. Hata hivyo, Ujumbe huo wa Umoja wa Afrika ulikutana kwa mazungumzo Alhamisi alaasiri na wawakilishi wa dini na asasi za kiraia, lakini pia wanasiasa.

Hata kama Utawala haujaeleza lolote, tayari, upinzani, umeanza kuonyesha msimamo wake na kusema kuwa hauna imani na Ujumbe huo kwani unaegemea upande wa utawala.

Ujumbe wa Umoja wa Afrika unaundwa na marais wa Afrika Kusini, Mauritania, Senegal, Gabon na waziri mkuu wa Ethiopia. Alhamisi hii, Rais Jacob Zuma ndiye aliendesha mashauriano yaliodumu saa mbili. Chama tawala cha CNDD-FDD na vyama vya siasa vinavyounga mkono utawala wa Bujumbura upande mmoja, na watu wengine wawili, upande mwengine, ambao ni viongozi wa FRODEBU na UPRONA, wawakilishi wa upinzani wachache ambao hawakukimbilia uhamishoni, wameshiriki mazungumzo hayo.

Baada ya mazungumzo hayo ya siku ya kwanza vyama vinavyounaga mkono utawala wa Bujumbura ikiwa ni pamoja na cha tawala cha CNDD-FDD havikutaka kueleza lolote. Mamlaka kwa upande wake, inasubiri kwanza kukutana na Rais Nkurunziza kabla ya kujieleza. Upinzani, hata hivyo, umekata tamaa.

Upinzani watwika lawama Ujumbe wa AU

Charles Nditije, kiongozi wa chama cha UPRONA, kisiotambuliwa na utawala, ameutuhumu Ujumbe wa Umoja wa Afrika kwamba mekuja kuthibitisha kubaki madarakani kwa Pierre Nkurunziza. Kwa mujibu wa Rais wa UPRONA, Jacob Zuma anasadikiwa kuwa ameweka kando swala la muhula wa tatu katika ajenda ya mazungumzo, na kuwataka wapinzani kuheshimu uamuzi uliopingwa awali na Mahakama ya Katiba, lakini hatimaye ikahalalisha kugombea kwa Pierre Nkurunziza.

"Hakuna jambo thabiti lililopendekezwa ili kukomesha machafuko yanayoendelea, ama mazungumzo. Wala hakuna tarehe iliyotolewa kwa mazungumzo, lakini viongozi hao wamesisitiza haja kuwashirikisha wapinzani wote katika mazungumzo," Charles Nditije amesema.

Mmoja kati ya wajumbe wa Umoja wa Afrika, amekataa kwa upande wake, kuwa wanaegemea upande wa utawala: "majadiliano yanaendelea na tutajaribu kuafikiana kuhusu mazungumzo yatakayowashirikisha wadau wote katika suala nzima la usalam na amani nchini Burundi", chanzo hiki kimeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.