Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-BAN-MAZUNGUMZO

Burundi: Rais Nkurunziza ajikubalisha kuanza mazungumzo na pande zote

Jumanne hii, Februari 23, Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ambaye nchi yake imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa kwa karibu miezi kumi amejikubalisha kuanza "mazungumzo" na upinzani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza mjini Bujumbura Jumanne hii.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (kulia) na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika mkutano na waandishi wa habari, Jumanne hii Februari 23 mjini Bujumbura.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (kulia) na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika mkutano na waandishi wa habari, Jumanne hii Februari 23 mjini Bujumbura. © REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Ban Ki-moon amehakikisha kwamba Rais wa Burundi amejikubalisha kuanzisha mazungumzo bila masharti yatakayozishirikisha pande zote husika katika siasa ya Burundi. Pande, zote ispokua wale wanaohusika katika vitendo vya kuzorotesha usalama wa nchi, amesema rais wa Burundi.

Hii ina maana kwamba baadhi ya wapinzani hawatashiriki katika mazungumzo, kwa maana utawala unawatuhumu kuhusika katika vurugu ambazo zinaendelea kulikumba taifa la Burundi. Hakuna uhakika kwamba wadau wote watasikilizwazinasikika. Viongozi wanapaswa kuonyesha nia njema, kwa mujibu wa Ban Ki-moon, ya ujasiri na uaminifu kwa kuanzisha mchakato wa kisiasa na kuhakikisha uheshimishwaji wa haki za binadamu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha maamuzi ya hivi karibuni ya Rais Nkurunziza: kuondoa vikwazo dhidi ya vyombo vya habari vya kibinafsi na vibali vya kukamatwa viliokua vimewekwa dhidi ya watu 15 ikiwa ni pamoja na wapinzani na waandishi wa habari, huku akibaini kwamba maamuzi hayo yanapaswa kufuatwa na hatua nyingine.

Katika mkutano wake na Ban Ki-moon, Rais wa Burundi pia ameahidi kuachia huru wafungwa 2,000, ambao bado haijafahamika ni wafungwa wa aina gani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.