Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-MAZUNGUMZO-USALAMA

Ujumbe wa Umoja wa Afrika ziarani Burundi

Siku mbili baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ujumbe wa marais na viongozi wa serikali watano wanaotumwa na Umoja wa Afrika unatarajiwa Alhamisi hii mjini Bujumbura.

Rais wa Senegal Macky Sall akipokelewa na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunia, Jumatano Februari 24, 2016.
Rais wa Senegal Macky Sall akipokelewa na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunia, Jumatano Februari 24, 2016. © RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Marais wa Senegal, Afrika Kusini, Gabon na Mauritania pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia watajaribu kutafuta ufumbuzi wa mgogoro unaoikabili nchi hii kwa miezi kumi sasa. Lengo la ziara hii: kumshawishi Rais Nkurunziza kukubali mazungumzo bila masharti na upinzani wote. Lakini suala la kupelekwa kwa askari wa Maprobu, kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Burundi, halimo katika ajenda ya mazungumzo baina ya viongozi hao.

"Viongozi watano kutoka nchi za Afrika waliotumwa na Umoja wa Afrika (AU) watasafiri Alhamisi watakuwa ziarani nchini Burundi ili kuendeleza mazungumzo kati ya wadau mbalimbali juu ya mgogoro wa kisiasa nchini humo tangu Aprili mwaka 2015," Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema Jumanne hii.

"Kwa ombi la Idriss Deby Itno, Rais wa Umoja wa Afrika, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ataongoza ujumbe wa viongozi wa nchi na serikali mjini Bujumbura tarehe 25 na 26 Februari 2016," ilisema taarifa hiyo. Mwishoni mwa mwezi Januari, Umoja wa mataifa ulikataa kutuma kikosi cha kulinda amani nchini Burundi, na kuamua badala yake kutuma haraka "Ujumbe wa ngazi ya juu" ili kuendeleza mazungumzo.

Jacob Zuma ataongozana na maafisa wanne: Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, Rais wa Senegal Macky Sall, Rais wa Gabon Ali Bongo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Ujumbe huu unatarajiwa kukutana na "viongozi wa ngazi ya juu wa Burundipamoja na wadau wengine kwa mashauriano juu ya mazungumzo baina ya Warundi," Ofisi ya Ikulu ya Pretoria imeongeza.

Afrika Kusini yatuma wanajeshi kwa ulinzi wa Ujumbe wa AU

Tayari wanajeshi kadhaa kutoka Afrika Kusini wameingia Jumanne hii wakiwa na magari ya kijeshi na zana za kivita kwa ulinzi wa viongozi hao wa Afrika ambao wanatazamiwa kuwasili mjini Bujumbura Alhamisi wiki hii, chanzo cha kidiplomasia kimebaini.

Siku ya Jumatatu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliwasili Bujumbura ili kujaribu kupata ufumbuzi wa mgogoro, wakati ambapo vurugu zikiendelea.

Usiku wa Jumatatu na Jumanne, kulitokea milipuko kumi ya maguruneti katika maeneo kadhaa ya mji mkuu Bujumbura na kusababisha watu wengi kujeruhiwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye ni kwa mara ya kwanza anafanya ziara ya kikazi nchini Burundi tangu nchi hii kutumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa mwezi Aprili mwaka 2015, aliweza kumshawishi Rais Nkurunziza kuanza mazungumzo ya amani na upinzani.

Kwa upande wake Rais Pierre Nkurunziza aliahidi Jumanne hii kuanza mazungumzo na wadau wote ispokua wale ambao wanahusika na mdororo wa usalama nchini Burundi, Ban Ki-moon amesema, kabla ya kuendelea na safari yake katika mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Muungano wa wanasiasa walio uhamishoni CNARED, kupitia naibu msemaji wake Pancrace Cmpaye, umesema hauna imani na kile kitakachotokea katika ziara hiyo ya viongozi wa Afrika, kwani marais wengi wa Afrika wamekua na dhamira ya kufanyia marekebisho katiba ili wasalie madarakani.

Rais wa Senegal Macky Sall akipokelewa na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunia, Bujumbura, Jumatano Februari 24, 2016.
Rais wa Senegal Macky Sall akipokelewa na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunia, Bujumbura, Jumatano Februari 24, 2016. © RFI-KISWAHILI

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.