Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: Hollande awataka wanajeshi kukabidhi madaraka kwa raia

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amelitaka jeshi la Burkina Faso kurejesha madaraka haraka iwezekanavyo kwa raia wa nchi hiyo ili pawepo na uchaguzi huru kwa ajili ya kuwapata viongozi halali wapya.

Rais wa Ufaransa François Hollande, akiwa katika mji wa Québec akitoa msimamo wa Ufaransa kuhusu hali inayoendelea Burkina Faso, Novemba 3 mwaka 2014.
Rais wa Ufaransa François Hollande, akiwa katika mji wa Québec akitoa msimamo wa Ufaransa kuhusu hali inayoendelea Burkina Faso, Novemba 3 mwaka 2014. REUTERS/Mathieu Belanger
Matangazo ya kibiashara

Tofauti na Marekani, ambayo ni mshirika mwingine wa karibu wa Burkina Faso iliyolitaka jeshi la nchi hiyo kukabidhi madaraka kwa raia, Ufaransa kwa upande wake ilikaribisha Ijumaa Oktoba 31 kuondoka mamlakani kwa amani kwa rais Blaise Compaoré kufuatia maandamano ya raia ambao waliandamana wakipinga marekebisho ya Katiba na kumtaka rais huyo ajiuzulu.

Rais François Hollande ambaye yuko ziarani Canada ameelezea msimamo wake kuhusu jinsi hali inavyoendelea nchini Burkina Faso. Rais Hollande amelitaka jeshi kuachia ngazi na kukabidhi raia madaraka ya uongozi wa nchi.

Rais François Hollande, amesema, alimsihi mara kadhaa rais Blaise Compaoré kutogombea muhula mwengine bila mafaanikio.

“Tangu mwanzoni mwa mgogoro huo, Ufaransa ilimuonya Blaise Compaoré. Hata hivo wakati wa maandamano ya kwanza, tulimtumia ujumbe mwengine kama huo”, amesema rais Hollande.

Wakati rais Blaise Compaoré alipokua akitafuta sehemu ya kukimbilia, Ufaransa iliingilia kati na kumuondoa nchini Burkina Faso.

“ Ufaransa na mataifa mengine yalilazimika kumuondoa Blaise Compaoré nchini Burkina Faso, ili damu zisiendeleyi kumwagika”, ameongeza rais Hollande.

Wakati hayo yakijiri, Umoja wa Afrika kwa upande wake umetoa kipindi cha majuma mawili kwa jeshi hilo kurejesha uongozi kwa raia wakati huu ambapo upatanishi wa kimataifa umewasili siku ya Jumatatu mjini Ouagadougou.

Umoja wa Afrika umetishia kuwawekea vikwazo viongozi wa kijeshi ikiwa agizo lao halitatekelezwa ndani ya muda uliyotolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.