Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: Zida akutana na wanasiasa

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa Jumapili Novemba 2 katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou, ambapo vikosi vya usalama vililazimika kufyatua risase hewani baada ya waandamanaji kujaribu kuingia katika majengo ya televisheni ya serikali ORTB.

Mkutano kati ya wawakilishi wa upinzani na luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougou Novemba 2 mwaka 2014.
Mkutano kati ya wawakilishi wa upinzani na luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougou Novemba 2 mwaka 2014. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalikua yaliitishwa na upinzani ukipinga jeshi kuchukua mamlaka ya uongozi wa nchi. Katika maandamano hayo mtu mmoja aliuawa. Wakati huohuo Luteni Kanali Zida aliye pewa na jeshi mamlaka ya uongozi wa nchi alikutana na wanasiasa wote mjini Ouagadougou kwa lengo la kupatia ufumbuzi maandamano na machafuko vinavyoendelea. Hata hivyo upinzani umesema utajieleza Jumatatu Novemba 3.

Katika mkutano na waandishi wa habari, kanali Barry, aliye zungumza kwa niaba ya luteni kanali Isaac Zida, amethibitisha kifo cha mtu mmoja wa vurugu ziliyotokea Jumapili Novemba 2 kwenye makao makuu ya televisheni ya taifa.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya na mabolozi wa Marekani na Ubelgiji walikutana Jumapili Novemba 2 na luteni kanali Isaac Zida. Hayo yanajiri wakati Umoja wa Ulaya uliomba hivi karibuni jeshi la Burkina Faso kuheshimu haki za raia, hasa kuwapa raia mamlaka ya uongozi wa nchi pamoja na kuandamana.

Jeshi limefahamisha kwamba litaendelea Jumatatu Novemba kukutana na viongozi wa dini mbalimbali, wakuu wa koo mbalimbali pamoja na mabalozi wa nchi za kigeni wanaowakilisha nchi zao nchini Burkina Faso.

Mkutano kati ya Luteni Kanali Zida na wawakilishi wa wanasiasa umefanyika katika makao makuu ya Baraza la Uchumi na Jamii (CES) mjini Ouagadougou, shirika la habari Burkina24. Baada ya kukutana na waandishi wa habari, Isaac Zida, ambaye amepewa mamlaka na jeshi ya kuliongoza taifa la Burkiana Faso alirejea ukumbini kukutana na ujumbe mkubwa wa wanasiasa, hususuan wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.