Pata taarifa kuu

Burkina Faso:mpasuko miongoni mwa wakuu wa kijeshi kuhusu kutawala nchi

Mpasuko umeibuka nchini Burkina Faso kati ya majeshi ya nchi hiyo juu ya nani wa kuiongoza nchi hiyo kufuatia kujiuzulu kwa raisi Blaise Compaoré baada ya kutawala kwa takribani miaka 27 nchini humo.

Jenerali Honoré Traoré(kushoto) na luteni kanali Isaac Zida (kulia) , kila mmoja ajitangaza rais wa Burkina Faso, baada ya kujiuzulu kwa Blase Compaoré
Jenerali Honoré Traoré(kushoto) na luteni kanali Isaac Zida (kulia) , kila mmoja ajitangaza rais wa Burkina Faso, baada ya kujiuzulu kwa Blase Compaoré REUTERS/Joe Penney-RFI
Matangazo ya kibiashara

Kamanda aliyeongoza ulinzi wa raisi kanali Isaac Zida, amesema kuwa anaendeleza kusimamia nchi kama mkuu wa serikali nchini humo.

Mapema mkuu wa majeshi General Honore Traoré alitangaza kushika madaraka ya nchi hiyo.

Umati wa raia ulionekana ukishangilia kwa furaha katika mji mkuu wa Ouagadougou, baada ya tangazo la kujiuzulu kwa raisi Compaoré.

Uamuzi wa rais Compaoré ulikuja baada ya masaa kadhaa kupita toka atangaze kutokuwa tayari kujiuzulu nafasi hiyo licha ya shinikizo na maandamano ya wananchi ambao wanapinga kiongozi huyo kujiongezea muda wa kukaa madarakani.

Kanali Boureima Farta ambaye alitangaza jeshi kuchukua mamlaka, amesema kuwa kwasasa rais Blaise Compaore na familia yake wameondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo Ouagadougou.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amepongeza uamuzi wa rais Compaoré ambapo mapema aliamini kuwa kiongozi huyo angeondoka madarakani kwa hiari.

Jumuiya ya kimataifa inataka kuwepo kwa hali ya utulivu wakati huu jeshi likichukua nchi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.