Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: muda wa kujua ukweli kuhusu Blaise Compaoré

Baada ya machafuko yaliyoanza tangu Alhamisi Oktoba 30 nchini Burkina Faso, Blaise Compaoré ameapa kutoachia madaraka hadi uchaguzi utakapofanyika.

Jeshi la Burkina Faso likijianda kuwatawanya waandamanaji, Oktoba 30 mwaka 2014, katika mji wa Ouagadougou.
Jeshi la Burkina Faso likijianda kuwatawanya waandamanaji, Oktoba 30 mwaka 2014, katika mji wa Ouagadougou. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo ameonekana Alhamisi jioni wiki hii kwenye televisheni, akitangaza kwamba haondoki madarakani. Blaise Compaoré amekua akipendekeza kuanzisha mazungumzo na upinzani, jambo ambalo upinzani umetupilia mbali.

Hali ya utulivu ilirejea Alhamisi jioni Oktoba 30 katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, baada ya kutokea machafuko yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na wengine wengi kujeruhiwa.

Hata hivo ni vigumu kujua idadi sahihi ya watu walifariki katika vurugu hizo, kwani machafuko yalitokea nchi nzima.

Hali ya wasi wasi iliripotiwa Alhamisi jioni Oktoba 30, baada ya kutangazwa kuwa serikali na Bunge vimevunjwa, huku rais akitangaza kuwa hataondoka madarakani wakati ambapo jeshi likitangaza serikali ya “mpito”.

Vurugu hizo zilisababishwa na makabiliano ya vikosi vya usalama na waandamanaji ambao waliingia barabarani wakipinga uwezekano wa kuifanyia marekebisho Katiba ya taifa la Burkina Faso, baada ya serikali kutuma muswada wa sheria uhusuo marekebisho ya Katiba, ambao ungelijadiliwa na wabunge Alhamisi Oktoba 30 na baadaye kupitishwa au kupingwa.

Lakini kulikua na uwezekano muswada huo kupitishwa kwani chama madarakani kikiungwa mkono na vyama vingine vilikua na wabunge wengi ambao wangelazimika kuupitisha. Lengo la marekebisho hayo ilikua kumpa nafasi rais Blaise Compaoré ili aweze kugombea kwa muhula mwengine, baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka 27.

Ofisi ya manispa ya jiji na makao makuu ya chama cha CDP vilichomwa moto katika mji wa Bobo Dioulaso, ambao ni mji wa pili nchini Burkina Faso. Kwa mujibu wa mwalimu wa shule ya sekondari akihojiwa na RFI katika mji wa Bobo Dioulaso, vurugu ziliyotokea katika mji huo zilisababisha vifo vya watu watano

Wanajeshi walishikamana na raia waliyokua wakiandamana baada ya jeshi kutangaza kwamba limeivunja serikali na Bunge, jambo ambalo limeshangaza wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.