Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: makubaliano yafikiwa juu ya serikali ya mpito ya mwaka mmoja

Mazungumzo yaliyo endeshwa na marais wa Ghana, Nigeria na Senegal Jumatano jioni Novemba 5 katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou yamekamilika.

Marais wa tatu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi wakikutana kwa mazungumzo na Wadau katika mgogoro wa Burkina Faso , Novemba 2 mwaka 2014, Ouagadougou
Marais wa tatu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi wakikutana kwa mazungumzo na Wadau katika mgogoro wa Burkina Faso , Novemba 2 mwaka 2014, Ouagadougou AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Hata kama wameshindwa kuafikiana kupata jina la mtu ambaye ataongoza serikali ya mpito kulingana na mahitaji ya jumuiya ya kimataifa, wadau katika mgogoro huo wameweza kukubaliana kwa namna serikali hiyo ya mpito itakavyoundwa.

Wadau wote katika mgogoro wa Burkina Faso walishiriki katika mkutano huo wenye lengo la kupatiya ufumbuzi hali inayojiri wakati huu, baada ya aliye kuwa rais wa taifa hilo Blaise Compaoré kulazimishwa kujiuzulu mwishoni mwa juma liliyopita.

Wadau hao waliafikiana kuunda serikali ya mpito itakayoongoza taifa hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hata hivo waliafikiana kumteua haraka iwezekanavyo mtu atakaye shikilia kwa muda kiti cha rais, wadhifa ambao ni muhimu wakati huu taifa hilo likiendelea kushuhudia mvutano kuhusu nafasi hiyo.

Serikali hiyo ya mpito itahudumu kwa kipidi cha mwaka mmoja hadi wakati wa maadalizi ya chaguzi za rais na wa Wabunge Novemba mwaka 2015.

Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, viongozi wa kidini, wawakilishi wa vyama vya kiraia pamoja na jeshi wataendelea kukutana kwa mazungumzo ili kuafikiana kuhusu uuandwaji wa taasisi mbalimbali za uongozi wa nchi.

Rais wa Ghana John Dramani mahama amesema kwamba ana imani kuwa suala la uundwaji wa serikali ya mpito na taasisi zingine za uongozi wa nchi litapatiwa ufumbuzi.

Rais Dramani mahama amewapongeza raia wa Burkina faso huku akiwasihi kuendelea katika mchakato huo kwa lengo la kuimarisha na kudumisha demokrasia nchini mwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.