Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: Isaac Zida aendelea kupata shinikizo la kuachia ngazi

Marais Macky Sall wa Senegal, Goodluck Jonathan wa Nigeria na John Dramani Mahama wa Ghana wanatarajiwa kuwasili leo Jumatano Novemba 5 mjini Ouagadougou.

Luteni kanali Yakouba Isaac Zida aliye pitishwa na jeshi kwenye mamlaka ya uongozi wa nchi, Jumapili Novemba 2 mwaka 2014.
Luteni kanali Yakouba Isaac Zida aliye pitishwa na jeshi kwenye mamlaka ya uongozi wa nchi, Jumapili Novemba 2 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Marais wa mataifa hayo ambayo ni wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi wanajielekeza Burkina Faso ili kukutana na Luteni Kanali Yacouba Isaac Zida kabla ya mkutano wao wa kilele siku ya Jumanne mjini Accra nchini Ghana.

Wakati hayo yakijiri, jeshi ambalo linaendelea na mashauriano limekubali kukabidhi madaraka kwa raia ndani ya majuma mawili kama ilivyoagizwa na Umoja wa Afrika, licha ya baadhi ya waangalizi ambao hawaamini uwepo wa nia ya dhati ya jeshi hilo kurejesha madaraka haraka.

Ziara ya marais hao watatu nchini Burkina Faso iliandaliwa kupitia mazungumzo yaliyokua yakiongozwa na wajumbe wa Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa pamoja na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Cédéao). Hata hivo waangalizi wanaofuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Burkina Faso, wamebaini kwamba viongozi hao wa tatu walifanya kazi kubwa katika kurejesha hali ya utulivu nchini humo.

Wajumbe hao wa Umoja wa Afrika, wamerejelea msimamo wa Umoja huo dhidi ya luteni kanali Issac Zida, wakimuonya kua iwapo hatokabidhi madaraka kwa raia mnamo siku 15, hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi wa kijeshi akiwemo afisa huyo aliye pitishwa na jeshi kushikilia mamlaka ya uongozi wa nchi.

Luteni kanali Isaac Zida, amethibitisha kuwa yuko tayari kukabidhi madaraka kwa raia, huku akiendelea kukutana na wadau wote katika suala nzima maendeleo ya Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.