Pata taarifa kuu

Warusi wa kujitolea wanaopigania Ukraine wadai kushambulia kijiji kimoja nchini Urusi

Raia wa Urusi wanaojitolea ambao wanapigana kwa upande Ukraine walmesema siku ya Jumanne kwamba wameshambulia na kuchukua udhibiti wa Tiotkino, kijiji cha Urusi karibu na mpaka wa Ukraine, operesheni ya ardhini ambayo inakuja baada ya shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani katika maeneo mengi ya Urusi.

Magari ya dharura yakiteketea kwa moto katika jengo la nishati na mafuta katika mji wa Kstovo, karibu kilomita 450 mashariki mwa Moscow, kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani, Machi 12, 2024.
Magari ya dharura yakiteketea kwa moto katika jengo la nishati na mafuta katika mji wa Kstovo, karibu kilomita 450 mashariki mwa Moscow, kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani, Machi 12, 2024. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na uvamizi wa Urusi kwa miaka miwili, Kyiv hushambulia mara kwa mara maeneo ya Urusi kwa kutumia ndege zisizo na rubani, lakini uvamizi katika eneo la Urusi ni nadra sana. Hii pia inakuja siku chache kabla ya uchaguzi wa urais nchini Urusi ambapo Vladimir Putin atachaguliwa tena kwa ushindi kwa kutokuwepo kwa upinzani wowote.

"Tumevuka mpaka," kitengo kinachoitwa Jeshi la Uhuru wa Urusi kilisema asubuhi kwenye Telegram, kikirusha hewani video ambayo kunaonekana magari matatu ya kivita yakiendeshwa gizani kwenye njia moja ya kijijini. Muda mfupi baadaye, kitengo hicho kilidai "kuharibu" gari la kivita la Urusi katika kijiji cha Tiotkino, katika jimbo la Kursk, lililoko mashariki mwa Ukraine. Mwakilishi wa kitengo cha Warusi wanaojitolea kupigana upande wa Kyiv aamenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kwamba mapigano yalikuwa bado yanaendelea katika majimbo ya Belgorod na Kursk hadi katikati ya asubuhi.

Kitengo, kinachoitwa kikosi cha Sibir, kilitangaza kwenye Telegram: "Kama ilivyoahidiwa, tunaleta uhuru na haki katika ardhi yetu ya Urusi." "Mapigano makali yanaripotiwa kwenye ardhi ya Urusi," ameongeza. Kitengo hiki pia kimetoa wito kwa Warusi "kususia uchaguzi wa urais" wa Machi 15-16-17. "Tunaweza tu kubadilisha mambo kuwa bora tukiwa na silaha mkononi," amesema, akielezea uchaguzi huo kama hadithi ya kubuni.

Jeshi la Urusi limetangaza kwamba lilizuia mashambulizi mengi kutoka Ukraine wakati wa usiku na asubuhi, na kuhakikisha kwamba lilizuia uvamizi wowote katika ardhi ya Urusi. Vikosi vya jeshi "vimefaulu kuzima jaribio la serikali ya Kiev kupata mafanikio kwenye ardhi ya Urusi katika majimbo ya Belgorod na Kursk," Wizara ya Ulinzi imesema. Msemaji wa Kremlin, Dmitri Peskov, amehakikisha, kwa upande wake, kwamba jeshi la Urusi lilikuwa likifanya "kile kinachohitajika" kupigana dhidi ya mashambulizi yote ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.