Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yatekeleza mashambulizi mapya, Zelensky ataka mifumo zaidi ya ulinzi wa anga

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesisitiza tena Jumamosi Machi 2 wito kwa washirika wake wa Magharibi kuipatia Kiev mifumo zaidi ya ulinzi wa anga, na kwa haraka zaidi, baada ya mashambulizi ya Urusi ambayo yamesababisha vifo vya watu sita, kulingana na Kiev.

Waokoaji wanafanya kazi kwenye eneo la jengo la ghorofa la iliyoharibiwa vibaya kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Urusi huko Odessa, Machi 2, 2024.
Waokoaji wanafanya kazi kwenye eneo la jengo la ghorofa la iliyoharibiwa vibaya kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Urusi huko Odessa, Machi 2, 2024. © Oleksandr Gimanov / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi yaliyolenga mji wa bandari wa Bahari Nyeusi wa Odessa usiku wa kuamkia leo yamesababisha vifo vya watu wanne, akiwemo mtoto mdogo, na uharibifu wa jengo la ghorofa tisa, maafisa wamesema maafisa wa Ukraine. Watu wanane wamejeruhiwa katika shambulio hilo, kwa mujibu wa waokoaji wa Ukraine. Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha sakafu kadhaa za jengo zikiwa zimeporomoka kabisa.

Wakati huo huo, milipuko ya mabomu ilimuua mzee wa miaka 76 katika mkoa wa Kharkiv, karibu na mpaka wa Urusi, na mtu mwingine katika mkoa wa Kherson kusini, kulingana na mamlaka ya mkoa. "Urusi inaendelea kushambulia raia," amelalamika Rais wa Ukraine Zelensky kwenye mtandao wa kijamii. "Tunahitaji ulinzi zaidi wa anga kutoka kwa washirika wetu. Lazima tuimarishe ngao ya anga ya Ukraine ili kuwalinda vyema watu wetu dhidi ya ugaidi wa Urusi. Mifumo zaidi ya ulinzi wa anga na makombora zaidi ya mifumo ya ulinzi wa anga huokoa maisha," amedai.

Ushindi dhidi ya Urusi "unategemea washirika wetu"

Baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita, katika siku za hivi karibuni, kiongozi wa Ukraine amewahimiza mara kwa mara washirika wake wa Magharibi kutoa msaada wa kijeshi kwa haraka zaidi, akitoa wito haswa wa risasi, mifumo zaidi ya ulinzi wa anga na ndege za kivita. Hata hivyo, misaada ya Marekani bado imezuiwa katika Bunge la Congress kutokana na upinzani kati ya Republicans na Democrats, na nchi za Ulaya, ambazo uwezo wao wa uzalishaji ni mdogo, zinachelewa kutoa makombora zilizoahidi katika miezi ya hivi karibuni. Ushindi dhidi ya Urusi "unategemea nyinyi washirika wetu", Volodymyr Zelensky alionya washirika wake wa Magharibi siku chache zilizopita, ambao msaada wao ni muhimu kwa Kyiv, lakini ambao wamekuwa wakisita katika miezi ya hivi karibuni kuthibitisha bahasha mpya za bajeti kwa lengo hili.

Kulingana na Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Roustem Oumerov, nusu ya silaha kutoka nchi za Magharibi zilizoahidiwa kwa Kyiv zinawasilishwa kwa kuchelewa. Tatizo hili linaongeza uchovu wa askari wanaosiriki katika vita, vinavyodumu miaka miwili sasa, dhidi ya idadi kubwa ya wanajeshi wa Urusi.

Siku ya Jumapili jeshi la Wanahewa la Ukraine lilisema kwamba limenasa ndege 14 kati ya 17 za zisizo kuwa na rubani za "Shahed" zilizorushwa na Urusi. Kwa upande wake, vikosi vya Kiev viliripotiwa kutekeleza shambulizi lao la ndege zisizo na rubani usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, ambalo liliharibu jengo la makazi huko St. Pétersbourg.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.