Pata taarifa kuu

Ukraine: Raia watatu wauawa, kumi na wawili wajeruhiwa wakati wa shambulio la Urusi Donetsk

Mashariki mwa Ukraine, mashambulizi ya Urusi yamesababisha vifo vya watu watatu na kumi na wawili kujeruhiwa, afisa mmoja wa eneo hilo ametangaza siku ya Jumapili Machi 10, wakati mwanamke mmoja aliuawa katika shambulio la anga la Ukraine kwenye kijiji cha Urusi karibu na mpaka.

Kituo cha reli kiliharibiwa na kombora la Urusi katika mkoa wa Donetsk, Februari 25, 2024.
Kituo cha reli kiliharibiwa na kombora la Urusi katika mkoa wa Donetsk, Februari 25, 2024. AFP - ANATOLII STEPANOV
Matangazo ya kibiashara

"Wakati wa usiku," mkuu wa mko wa Donetsk, Vadym Filachkine, alisema jeshi la Urusi lilishambulia Dobropillia (mji ulio karibu kilomita 45 kutoka uwanja wa vita) na ndege zisizo na rubani za Shahed. Asubuhi, waokoaji walipata miili ya watu wawili chini ya vifusi vya nyumba. Kulingana na chanzo hiki, jeshi la Urusi pia lilishambulia kwa mizinga asubuhi ya Machi 10 mji wa Chassiv Yar, ulio karibu na uanja wxa vita katika mkoa wa Donetsk, na kuua mzee wa miaka 66. Makombora matatu ya jeshi la Urusi ya S-300 pia yalipiga mji wa Myrnograd - katika mkoa wa Donetsk - na kusababisha watu kumi na wawili kujeruhiwa kulingana na ripoti iliyosasishwa, ikiwa ni pamoja na kijana mmoja, amesema Vadym Filachkine. Majengo tisa ya ghorofa yaliharibiwa katika shambulio hilo, amengeza.

Ndege zisizo na rubani thelathini na tano zadondoshwa

Jeshi la Wanahewa la Ukraine pia limesema siku ya Jumapili kwamba limedungua ndege 35 zisizo na rubani za Shahed zilizotengenezwa na Iran, kati ya jumla ya 39 zilizorushwa na Urusi usiku kucha katika mikoa kumi ya kati na kusini mwa Ukraine. Nchini Urusi, mwanamke ameuawa siku ya Jumapili Machi 10 katika shambulio la bomu la Ukraine lililolenga kijiji cha Urusi kilichoko kilomita kumi kutoka mpakani, afisa wa eneo hilo amesema. "Leo, kijiji cha Kulbaki kililipuliwa kwa bomu kutoka Ukraine," amesema gavana wa jimbo la Kursk, Roman Starovoit. "Moto ulizuka katika jengo la ghorofa. Mwanamke mmoja amefariki na mumewe amejeruhiwa vibaya baada ya kuungua. "

Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia imeripoti ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine zilizoharibiwa katika eneo la Belgorod. Siku ya Jumamosi Machi 9, Urusi ilidai kuharibu ndege 47 za Ukraine wakati wa usiku, haswa katika eneo la Rostov-on-Don, linalopakana na Ukraine, shambulio ambalo liliweza kulenga, pamoja na mambo mengine, kiwanda cha kutengeneza vifaa vya ndege za jeshi. Ukraine hufanya mashambulizi ya anga mara kwa mara nchini Urusi, haswa katika mikoa iliyo karibu na eneo lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.