Pata taarifa kuu

Watu 100,000 waandamana London wakitaka 'kukomeshwa kwa vita Gaza'

Makumi kwa maelfu ya watu wameandamana mjini London Jumamosi alasiri kutaka "kukomeshwa kwa vita huko Gaza" na kuwaunga mkono Wapalestina, wiki mbili baada ya shambulio la umwagaji damu la Hamas nchini Israel ambalo lilisababisha jibu kali katika Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji wameandamana kuelekea Whitehall, katikati mwa mji mkuu wa Uingereza.
Waandamanaji wameandamana kuelekea Whitehall, katikati mwa mji mkuu wa Uingereza. AP - David Cliff
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji waliokuja katika makundi madogo au familia walimiminika kwa maelfu katika wilaya ya Marble Arch katikati mwa London. Msafara huo kisha ulianza kuelekea Whitehall, barabara inayoelekea Downing Street, huku wakiimba bila kuchoka "muiachie huru Palestine", wakiwa na bendera na mabango mengi ya Palestina, ambayo yalikuwa yameandikwa "Gaza: Acha mauaji" au "Komesha uvamizi". Takriban saa nane mchana, mkusanyiko huo ulijumuisha karibu watu 100,000, polisi wa London imesema kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

"Tulikuja kutoa msaada wetu, kwa sababu hatuwezi kukaa kimya, kutazama habari na kutofanya lolote," Mariam Abdul-Ghani, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 ambaye familia yake ina asili ya Palestina, ameliambia shirika la habari la AFP. "Nina binamu, familia na marafiki (huko)," Nivert Tamraz, mshauri wa masoko mwenye umri wa miaka 38, ambaye alikuja na watoto wake kuwaonyesha "kwamba wakati mwingine tunapaswa kupigania ubinadamu wetu." na msijifanye kutokujali.” "Pia nina rafiki ambaye familia yake iko Gaza, hawezi hata kupata habari zao, ni mbaya sana, hajui kama wamekufa au wako hai," ameongeza.

"Kwetu sisi, ni muhimu kuwa hapa ili kuonyesha mshikamano wetu na kupinga wazo kwamba ni Waislamu dhidi ya Wayahudi, Wapalestina dhidi ya Waisraeli," David Rosenberg, 65, mwanachama wa kundi la wanasoshalisti wa Kiyahudi kutoka London amesema. "Kuna watu hapa ambao wana umri wa miaka 20 na 30, ambao walikulia katika nyumba za jadi za Kiyahudi, na ambao hawawezi kustahimili kile kinachopaswa kufanywa kwa jina lao," ameongeza.

Mwisho wa maandamano kwa amani

Zaidi ya watu 1,400 waliuawa katika ardhi ya Israel wakati wa shambulio lililotekelezwa tarehe 7 Oktoba na kundi la wanamgambo  wa Kiislamu la Hamas. Wengi wao ni raia waliouawa kwa risasi, kuchomwa moto wakiwa hai au wamekufa kutokana na ukeketaji, kulingana na mamlaka ya Israel. Katika Ukanda wa Gaza, zaidi ya Wapalestina 4,300, wengi wao wakiwa raia, waliuawa katika kujibu mashambulizi ya jeshi la Israel, kulingana na wizara ya afya ya Hamas huko Gaza. Msafara wa kwanza wa misaada ya kibinadamu kutoka Misri uliingia Ukanda wa Gaza siku ya Jumamosi, ukisubiriwa kwa hamu na wakaazi wake waliozingirwa ambao wamekosa kila kitu kwa siku kadhaa.

Kama wiki iliyopita, maandamano hayo yaliwekwa chini ya uangalizi wa hali ya juu, na maafisa wa polisi elfu moja mitaani na helikopta ikiruka juu ya eneo kulikuwa kukifanyika maandamano hayo. Wakati maandamano yalipowasili Whitehall, waandamanaji walitawanyika kwa utulivu mchana, polisi ya London mesema. Uhamasishaji mwingine pia ulifanyika Jumamosi huko Birmingham, katikati mwa Uingereza, Dublin na Cardiff huko Wales, na pia katika miji mingine ya Ulayaa. Jumamosi ya wiki iliyopita, maelfu ya watu walifanya maandamano mjini London kuwaunga mkono Wapalestina. Watu kumi na watano walikamatwa kwa "makosa mbalimbali", Scotland Yard ilisema.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.