Pata taarifa kuu

Vita vya Hamas-Israel: Idadi ya vifo vya Wafaransa yaongezeka mateka wawili waachiliwa

Mwanamke, raia wa Marekani na binti yake waliweza kuondoka Ukanda wa Gaza, baada ya kuachiliwa na wanamgambo wa Hamas waliokuwa wanawashikilia mateka. 

Picha ya kumbukumbu isiyo na tarehe ya Judith Raanan (kushoto) na bintiye Natalie, iliyotolewa na familia kwa vyombo vya habari. Mateka wa Hamas, waliachiliwa Ijumaa hii, Oktoba 20, 2023.
Picha ya kumbukumbu isiyo na tarehe ya Judith Raanan (kushoto) na bintiye Natalie, iliyotolewa na familia kwa vyombo vya habari. Mateka wa Hamas, waliachiliwa Ijumaa hii, Oktoba 20, 2023. © Courtesy of Raanan family via AP
Matangazo ya kibiashara

Mateka wa Hamas tangu shambulio la kigaidi la Oktoba 7, raia hao wawili wa Marekani wameachiliwa "kwa sababu za kiutu, kufuatia upatanishi kutoka Qatar na kuwathibitishia watu wa Marekani na ulimwengu kwamba matamshi ya Bw. Biden na utawala wake wa kifashisti ni ya uongo na hayana msingi wowote," msemaji wa kijeshi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas amesema katika taarifa. Habari iliyothibitishwa na vyombo vya habari vya Israeli. 

Takriban mateka 200 wa Israel, wageni au watu wenye uraia pacha walitekwa nyara nchini Israel na kupelekwa Gaza na wapiganaji wa Hamas.

Wafaransa thelathini wameuawa

Idadi ya raia wa Ufaransa waliouawa katika mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel imefikia 30. Idadi hiyo imeongezeka tena, Wizara ya Mambo ya Nje imetangaza Ijumaa. "Ufaransa inasikitishwa na kifo cha kutisha cha raia mwingine wa Ufaransa, ambacho kinafanya idadi ya wahanga wa Ufaransa kufikia 30" katika mashambulio haya, imesema taarifa kutoka Quai d'Orsay, wizara ya mambo ya Nje ya Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.