Pata taarifa kuu

Volodymyr Zelensky atembelea wanajeshi wake walio vitani mashariki mwa Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametangaza siku ya Jumanne kwamba ametembelea wanajeshi wake walio vutani Mashariki mwa nchi, katika eneo la majimbo ya Kupiansk na Lyman, linalokumbwa na mashambulizi ya vikosi vya jeshi la Urusi.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy akitembelea eneo la Ukumbusho la Mashujaa waliouawa katika vita vya Ukrainedhidi ya uvamizi wa Urusi, Ukraine mjini Kyiv, Ukraine Oktoba 1, 2023.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy akitembelea eneo la Ukumbusho la Mashujaa waliouawa katika vita vya Ukrainedhidi ya uvamizi wa Urusi, Ukraine mjini Kyiv, Ukraine Oktoba 1, 2023. via REUTERS - UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SER
Matangazo ya kibiashara

"Leo tumetembelea brigedi zetu zinapambana katika moja ya maeneo yenye vita zaidi, Kupiansk na Lyman," Volodymyr Zelensky ameandika kwenye Telegram, akirusha video ambayo anaweza kuonekana akiwa pamoja na askari katika kile kinachoonekana kama makazi yalliyo chini ya ulinzi mkali.

Rais wa Ukraine amesema "amejadili operesheni katika uwanja wa vita, masuala ya sasa na mahitaji na makamanda wa vitengo vya jeshi na wanajeshi." Kulingana na mkuu wa utawala wa rais Andriï Iermak, Volodymyr Zelensky pia ametunuku askari na "akagua vifaru aina ya Leopard 2 na magari ya vikosi vya ardhini aina ya CV-90", yaliyotolewa na nchi za Magharibi kwa Kiev kwa mashambulizi yake dhidi ya Urusi na ambayo "yalitumiwa katika vita katika eneo la Kupiansk”.

Biden ahakikisha juu ya uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine

Joe Biden alifanya mkutano kwa nji ya simu siku ya Jumanne na viongozi kadhaa wa nchi zinazoshirikiana na Marekani "kuratibu msaada zaidi kwa Ukraine," Ikulu ya White imesema katika taarifa fupi.

Rais wa Marekani alizungumza, kwa mujibu wa chanzo kimoja, na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen, rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, rais wa Poland Andrzej Duda, rais wa Romania Klaus Iohannis, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna.

Jens Stoltenberg alizungumza kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ikiitwa Twitter) kuhusu "mazungumzo mazuri" na kuongeza: "Tunaahidi kuunga mkono Ukraine kwa muda mrefu ikiwa itahitajika."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.