Pata taarifa kuu

Marekani kuendelea kuisaidia Ukraine

NAIROBI – Lazima tuhakikishe Urusi inakuwa taifa la mwisho kutumia mabavu kutawala nchi nyingine, ni ujumbe wa rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky kwa viongozi wa nchi za G7 waliokutana nchini Japan mwishoni mwa juma lililopita.

Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy pembeni ya mkutano wa G7 nchini Japan, Jumapili, Mei 21, 2023. (AP Photo/Susan Walsh)
Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy pembeni ya mkutano wa G7 nchini Japan, Jumapili, Mei 21, 2023. (AP Photo/Susan Walsh) AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wenzake, Zelensky, amesisitiza umuhimu wan chi yake kuendelea kupewa silaha zaidi kukabiliana na Urusi aliyoiita mvamizi.

Kwa upande wake rais wa Marekani, Joe Biden, amesema nchi yake itaendelea kusimama na Ukraine kuhakikisha mwishowe inashinda vita dhidi ya uvamizi wa Moscow.

‘‘Kwa pamoja na nchi washirika kwa mara nyengine tumesisitiza umuhimu wa amani ambayo itaheshimu uhuru wa Ukraine na mipaka yake.’’ Alisema rais Joe Biden.

00:38

Rais Joe Biden kuhusu msaada kwa Ukraine

Rais Biden aidha katika hotuba yake alieleza Urusi ndiyo ambayo iliaanzisha vita hivyo na inauwezo wa kuvimaliza hata sasa hivi kwa kuwaondoa wanajeshi wake huko Ukraine na kuachia mipaka inayoshikilia pamoja na kuacha mashambulio.

Viongozi hao wameeleza kuendelea kuisaidia nchi ya Ukraine kiuchumi, kibindamu na kiusalama iliendelea kusimama imara kadiri inavyowezekana.

Marekani imetangaza msaada mwengine wa roketi, risasi, roketi za kudungua vifaru kama njia moja ya kuisaidia Ukraine katika uwanja wa mapambano.

Rais wa Ukraine alikuwa miongoni mwa viongozi waliokutana katika kikao cha wakuu wa nchi za G7 nchini Japan
Rais wa Ukraine alikuwa miongoni mwa viongozi waliokutana katika kikao cha wakuu wa nchi za G7 nchini Japan © AP / Stefan Rousseau

Katika hatua nyengine rais Biden, hivi leo anatarajiwa kukutana na spika wa bunge la Congress, Kevin McCarthy, kwa raundi nyingine ya mazungumzo kujaribu kumaliza mvutano kuhusu hatua za kuchukua kabla ya kuruhusu Serikali kukopa fedha zaidi.

Kwa majuma kadhaa, Biden amekuwa akivutana na spika huyu wa Republican, kuhusu namna ya kunusuru nchi hiyo kuwa mufilisi, rais Biden akisisitiza madai ya Republicans hayakubaliki.

‘‘Tulikubalina njia moja peke ya sisi kusonga mbele ni makubaliano ya pande zote, nimetimiza kwa upande wangu kwa kuweka mezani mapendekezo ambayo yatapunguza matumizi kwa zaidi ya dola trilioni moja." Alieleza rais Biden.

00:35

Rais Joe Biden kuhusu Deni

Hii si mara ya kwanza kwa Marekani kujikuta katika hali hii, ilishashuhudiwa pia wakati wa rais Barack Obama na Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.