Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Kyiv yazitaka nchi za Magharibi kuwasilisha vifaru vyao vizito haraka iwezekanavyo

Ukraine inatarajia kupokea vifaru vizito vilivyoahidiwa na Ujerumani na Marekani haraka iwezekanavyo, kasi ya uwasilishaji wao ni muhimu katika kukabiliana na mashambulizi ya Urusi, kulingana na Kyiv.

Baada ya wiki kadhaa za kusitasita, Marekani na Ujerumani zilitangaza siku ya Jumatano kuipa Ukraine vifaru vizito, kuonyesha msaada zaidi wa nchi za Magharibi kwa Kyiv katika matarajio ya uwezekano wa kukabiliana na uvamizi wa Urusi.
Baada ya wiki kadhaa za kusitasita, Marekani na Ujerumani zilitangaza siku ya Jumatano kuipa Ukraine vifaru vizito, kuonyesha msaada zaidi wa nchi za Magharibi kwa Kyiv katika matarajio ya uwezekano wa kukabiliana na uvamizi wa Urusi. AP - Philipp Schulze
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipongeza uamuzi wa nchi za Magharibi na kuweka kiwango cha juu zaidi kwa kudai makombora ya masafa marefu na ndege za kivita.

Kwa muda mfupi, "muhimu sasa ni kasi na kiasi" cha utoaji wa vifaru, amesema. Utoaji wa vifaru hivi ni "hatua muhimu kwa ushindi wa mwisho", aliongeza Volodymyr Zelensky katika hotuba yake ya kila siku siku ya Jumatano jioni. "Leo dunia huru imeunganishwa kuliko hapo awali kwa lengo moja: ukombozi wa Ukraine," alisisitiza.

Baada ya wiki kadhaa za kusitasita, Marekani na Ujerumani zilitangaza siku ya Jumatano kuipa Ukraine vifaru vizito, kuonyesha msaada zaidi wa nchi za Magharibi kwa Kyiv katika matarajio ya uwezekano wa kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Washington ilitangaza kutuma vifaru chapa Abrams 31, wakati Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliahidi kuipa Ukraine vifaru chapa Leopard 2, vifaru vizito ambavyo Kyiv imekuwa ikiomba kwa muda mrefu kukabiliana na vifaru vya kivita vya Urusi. "Hili sio tishio la mashambulizi dhidi ya Urusi," Rais wa Marekani Joe Biden alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.