Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Rais wa Marekani Joe Biden afungua njia ya kuikabidhi Ukraine ndege za F-16

Hii ni hatua muhimu ya mabadiliko katika uungwaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Kiev na uamuzi ulioelezwa kuwa wa "kihistoria" na Rais Volodymyr Zelensky: Joe Biden sasa yuko tayari kuruhusu nchi nyingine kuipatia Ukraine ndege za kivita inazoomba kwa haraka.

Rais Joe Biden sasa yuko tayari kuruhusu nchi nyingine kuipa Ukriane ndege aina ya F-16 zilizotengenezwa nchini Marekani.
Rais Joe Biden sasa yuko tayari kuruhusu nchi nyingine kuipa Ukriane ndege aina ya F-16 zilizotengenezwa nchini Marekani. © Esteban Felix / AP
Matangazo ya kibiashara

Joe Biden, ambaye anahudhuria mkutano wa kilele wa G7 nchini Japan, amewahakikishia washirika wake "kuunga mkono mpango wa pamoja wa kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kwa ndege za kivita za kizazi cha nne, ikiwa ni pamoja na ndege aina ya F-16", kulingana na afisa mkuu wa Ikulu ya White House.

Tangazo hilo lilikaribishwa haraka na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, pamoja na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo na Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi Kajsa Ollongren. "Uingereza itashirikiana na Marekani, Uholanzi, Ubelgiji na Denmark ili kuipa Ukraine uwezo wa anga inayohitaji kupambana dhidi ya Urusi," Rishi Sunak amesema. Hii "itasaidia sana jeshi letu la anga", amebainisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Joe Biden, ambaye ndiye anaongoza majibu ya nchi za Magharibi kwa Urusi, anakabiliwa na shinikizo kubwa la kuruhusu ndege ya Marekani ya Lockheed Martin kutumwa Ukraine, si kupitia Marekani yenyewe, bali na nchi nyingine ambazo zina ndege za aina hiyo. Kutumwa kwa ndege hizi na nyingine kunategemea idhini ya awali kutoka Washington, na hasa zaidi kwa idhini kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje, ili kulinda teknolojia ya kijeshi ya Marekani.

Hatua muhimu

"Mafunzo hayo yanapoendelea katika miezi michache ijayo, muungano wetu wa mataifa yanayoshiriki katika juhudi hizi utaamua wakati wa kutoa ndege, ngapi, na nchi gani zitazitoa," rais wa Marekani ameongeza. Utaratibu huu - 'wakati' na sio 'ikiwa' - ni, kutoka Marekani, ishara nzuri zaidi hadi sasa kwa utoaji wa vifaa hivi ambavyo Kyiv inahitaji.

Volodymyr Zelensky amekuwa akiwaomba washirika wake wa Magharibi kwa miezi kadhaa kumpatia ndege ambazo zingeruhusu jeshi la Ukraine kuwashambulia kwa kina wanajeshi wa Urusi, bila hata hivyo kutengeneza suluhu la muujiza katika mzozo huo.

Siku ya Jumanne, Uingereza iliomba kuwepo kwa "muungano wa kimataifa" unaonuia kusambaza ndege hizi za kivita kwa jeshi la Ukraine, lakini wakati huo ilibaini, kwa kushirikiana na Ujerumani, kwamba ni 'White House' kutoa idhini ya mwisho. Poland, ambayo ina ndege aina ya F-16, tayari imeonyesha kuwa itakuwa tayari kuzotoa kwa Ukraine, kama ilivyo kwa Uholanzi ambayo, kama nchi kadhaa za NATO, imefanya kubadili nafasi ya meli zao za F-16 kwa ndege mpya za  F-35.

Denmark imetangaza kuwa itawasaidia marubani wa Ukraine kutumia ndege ya kivita ya F-16 iliyotengenezwa Marekani, tangazo lililotolewa na Kaimu Waziri Troels Lund Poulsen. "Denmark itafanya kila juhudi kufanya mchango huu wa kipaumbele," alisema. Hata hivyo, hakubainisha iwapo Denmark itchangia kwa utoaji wa baadhi ya vifaa hivyo.

Kwa sasa, hakuna suala la Marekani kufanya uamuzi kama huo peke yake, lakini kuruhusu tu nchi nyingine kufanya hivyo itakuwa hatua kubwa ya mabadiliko katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi wa mwezi Februari 2022. Ikulu ya White House yenyewe imekuwa ikirekebisha msimamo wake mara kwa mara tangu mwanzo wa vita. Hivi karibuni iliidhinisha kutumwa kwa vifaru vya Marekani kwa Ukraine, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa mwiko huko Washington.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.