Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI

Ukraine: Raia zaidi waokoloewa kutoka Mariupol

Raia zaidi yameripotiwa kuondolewa kutoka kwenye kiwanda cha kutengeneza chuma katika mji wa Mariupol baada ya shambulio liliotekelezwa na makombora ya jeshi la Urusi.

Mtoto akionekana akiwa na baba yake wakiondoka kwenye mji wa viwanda wa Azovstal, akisindikizwa na mwanajeshi wa Urusi. Mei 6, 2022.
Mtoto akionekana akiwa na baba yake wakiondoka kwenye mji wa viwanda wa Azovstal, akisindikizwa na mwanajeshi wa Urusi. Mei 6, 2022. AP - Alexei Alexandrov
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa Ukraine wamekuwa wakipigana kuulinda mji wa Mariupol kutochukuliwa na wanajeshi wa Moscow.

Taarifa kutoka kwa maofisa wa Urusi na wale wa Ukraine, wamedhibitisha kuwa watu 50 wameondolewa kwenye kiwanda cha Azovstal na kukabidhiwa rasimi kwa Umoja wa mataifa UN na shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.

Watoto 11 ni miongoni mwa watu waliondolewa kwenye kiwanda cha Azovstal kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Urusi.

 

Raia zaidi wa Ukraine kwenye mji wa Mariupol wakiendelea kuondolewa kwenye mji huo
Raia zaidi wa Ukraine kwenye mji wa Mariupol wakiendelea kuondolewa kwenye mji huo AP - Vadim Ghirda

Watu wengine 500 tayari walikuwa wameondolewa kwenye kiwanda hicho, maofisa wa Urusi kwa ushirikiano wa naibu waziri mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk wamedhibitisha kuwa zoezi shughuli ya kuwaondoa raia waliokwama ndani ya kiwanda hicho itaendelea leo jumamosi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, amesema kuwa mazungumzo ya kidplomasia kwa sasa yanaendelea ilikuwaondoa wapiganaji wake ambao wanagali ndani ya kiwanda hicho cha  Azovstal mjini Mariupol.

Wapiganaji wa Ukraine wanaohifiwa kuwa Urusi inapanga kuwamaliza kabla ya jumatatu ya wiki ijao siku ambao Moscow itakuwa inaadhimisha ushindi wa zilizokuwa nchi za kisovieti.

Haya yanajri wakati huu Rais wa Marekani, Joe Biden kwa Ushirikiano na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, Katika mawasiliano ya njia ya simu wakisisitiza msimamo wa mataifa hayo mawili kuwajibisha Urusi dhidi ya vitendo vyake vya kuivamia Ukraine.

Nayo wizara ya ulinzi ya Urusi imedhibitisha kuwa imeharibu shehena kubwa iliyokuwa imebeba silaha kutoka Marekani na mataifa mengine ya bara Uropa karibu na kituo cha treni cha Bohodukhiv kwenye mji wa Kharkiv nchini Ukraine.

Wizara hiyo aidha imesema imeharibu vifaa 18 vya wanajeshi wa taifa la Ukraine kwa usiku moja vikiwemo vituo vitatu vya kuhifadhi silaha katika eneo la Dachne, karibu na bandari ya Odesa.

Naye Vyacheslav Volodin mbunge wa ngazi ya juu nchini Urusi, akiituhumu Washington kwa kupanga operesheni za kijeshi nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.