Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Poland na Ukraine zatangaza makubaliano juu ya usafirishaji wa nafaka

Tangazo la Wizara ya Kilimo ya Poland ya makubaliano na Lithuania kuwezesha usafirishaji wa nafaka zinazozalishwa nchini Ukraine kupitia Poland ni hatua ya kwanza kuchukuliwa kati ya miji mikuu hii miwili tangu kuanza kwa mzozo wa kidiplomasia kati ya Kiev na Warsaw. Mkataba huu haumalizi kizuizi kilichoamriwa na Poland, lakini utaharakisha usafirishaji wa nafaka kwenda katika maeneo ambayo yanakabiliwa na uhaba wa nafaka hizo.

Nafaka iliyohifadhiwa kwenye bohari baada ya mavuno katika eneo la Odessa nchini Ukraine, Juni 23, 2022.
Nafaka iliyohifadhiwa kwenye bohari baada ya mavuno katika eneo la Odessa nchini Ukraine, Juni 23, 2022. © Igor Tkachenko/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Je, mvutano kati ya Warszaw na Kyiv kuhusu suala la nafaka ya Ukraine unakaribia kumalizika? Makubaliano ya pande tatu kwa vyovyote vile yametangazwa. Kufikia Jumatano hii, nafaka za Ukraine zilizokusudiwa kuvuka Poland hadi kufikia Lithuania sasa zitadhibitiwa na mamlaka ya Lithuania, katika bandari ya nchi hiyo, Robert Telus ameeleza.

Kulingana na Waziri wa Kilimo wa Poland, chaguo hili litaharakisha mchakato huo kwani hadi sasa ukaguzi huu ulifanyika kwenye mpaka wa Ukraine na Polande. Nafaka za Ukraine ambazo zitasafirishwa kwa nchi ambazo zinakabiliwa na uhaba wa nafaka, au kwa nchi zingine ambazo hazijaweka vikwazo vya nafaka hizi.

Warsaw inashikilia vikwazo vyake

Kwa sababu kama suala la usafiri sasa inaonekana kutatuliwa na mkataba huu, hii si kesi na uagizaji wa nafaka kutoka Ukraine nchini Poland. Warsaw haijabadilisha msimamo wake na bado inataka kulinda soko lake na wakulima wake dhidi ya kuporomoka kwa bei ya nafaka, kama ilivyokuwa kabla ya marufuku hiyo kutolewa katika msimu wa masika uliopita.

Vikwazo ambavyo viliondolewa katikati ya mwezi wa Septemba na Tume ya Ulaya, lakini Hungary, Slovakia na Poland hata hivyo ziliamua kuendeleza vikwazo hivyo. Mvutano kati ya Warsaw na Kyiv kwa hivyo haujaisha kabisa, hata kama makubaliano haya yatawezesha kuharakisha usafirishaji wa nafaka za Ukraine wakati nchi nyingi zinakabiliwa na uhaba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.