Pata taarifa kuu

Poland haitaki tena kutoa silaha kwa Ukraine, katikati ya mzozo wa nafaka

Poland imetangaza hivi punde Jumatano jioni kwamba hatatoa tena silaha kwa Kiev, taarifa inayoonyesha mvutano unaokua kati ya washirika hao wawili, katika kipindi muhimu cha mashambulizi ya Kiev kwa uvamizi wa Urusi.

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki, kushoto, na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa mazungumzo kama sehemu ya mkutano wa kilele wa EU huko Brussels mnamo Februari 2023.
Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki, kushoto, na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa mazungumzo kama sehemu ya mkutano wa kilele wa EU huko Brussels mnamo Februari 2023. AP - Geert Vanden Wijngaert
Matangazo ya kibiashara

"Hatutoi tena silaha za aina yoyote kwa Ukraine," amesema Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki kwenye televisheni ya kibinafsi ya Polsat News.

"Tunazingatia zaidi kulifanya jeshi la Poland kuwa la kisasa na kwa haraka, ili liwe moja ya majeshi yenye nguvu zaidi ya nchi kavu barani Ulaya, na kwa muda mfupi sana," ameongeza.

Pia amebainisha kuwa kituo cha kijeshi kilicho katika mji wa Rzeszow, kusini-mashariki mwa nchi, ambapo hupitia silaha za nchi za Magharibi kwenda Ukraine, kilikuwa kikifanya kazi kwa kawaida.

Waziri Mkuu hakutaja ni lini Poland, mojawapo ya wauzaji wakubwa wa silaha kwa Ukraine, ilipoacha kutoa, au ikiwa hii ilihusishwa na mzozo wa nafaka ya Ukraine, ambayo Warszaw imepiga marufuku uagizaji kutoka nje ili kulinda maslahi ya wakulima wake.

Tangazo lake linakuja saa chache baada ya Warsaw kumuitisha kwa "dharura" balozi wa Ukraine kupinga maoni ya Rais Volodymyr Zelensky katika Umoja wa Mataifa.

Siku ya Jumanne, rais wa Ukraine alikosoa "baadhi ya nchi ambazo zinajifanya kuwa na mshikamano (na Ukraine) kwa kuunga mkono Urusi kwa njia isiyo ya moja kwa moja."

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, ambaye alimpokea mwanadiplomasia wa Ukraine, alishutumu "tasnifu hii ya uwongo" na "hasa isiyo na sababu kuhusu Poland ambayo imeunga mkono Ukraine tangu siku za kwanza za vita".

Tangazo la Brussels siku ya Ijumaa la kusitisha marufuku ya uagizaji wa nafaka kutoka Ukraine ililootamkwa mnamo mwezi Mei na mataifa matano ya EU, liliamsha hasira, na kusababisha vikwazo vya upande mmoja ambapo Kiev ilijibu Jumatatu kwa kutangaza kuwasilisha malalamiko mbele ya Shirika la Biashara Duniani. (WTO).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.