Pata taarifa kuu

UN: Mkutano Mkuu wafunguliwa katika muktadha wa mizozo mingi

Vikao vya Mkutano Mkuu la Umoja wa Mataifa vimefunguliwa Jumanne Septemba 19, kwa hotuba kali kutoka kwa nchi wanachama, katika muktadha wa migogoro mingi ya kimataifa. Katikati ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kujitokeza kwa mara ya kwanza ana kwa ana kwenye jukwaa, muda mfupi baada ya hotuba ya mwenzake wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva. Lakini tahadhari pia inaelekezwa kwa Nagorno-Karabakh, ambapo Azerbaijan imezindua mashambulizi mapya.

Kikao cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kimefunguliwa Jumanne Septemba 19, kwa hotuba kadhaa kutoka kwa wakuu wa nchi, katika muktadha wa migogoro mingi, huko New York. Hapa, ni wakati wa hotuba ya Rais wa Marekani Joe Biden.
Kikao cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kimefunguliwa Jumanne Septemba 19, kwa hotuba kadhaa kutoka kwa wakuu wa nchi, katika muktadha wa migogoro mingi, huko New York. Hapa, ni wakati wa hotuba ya Rais wa Marekani Joe Biden. AP - Mary Altaffer
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipanda kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza tangu uvamizi wa Urusi, akikabiliana na jumuiya ya kimataifa iliyogawanyika na kutikiswa na migogoro mfululizo, hasa vita vya Ukraine. Mwaka mmoja uliopita, aliruhusiwa kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wa video.

Wakati huu, ameshiriki  ana kwa ana, kwa kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne na mkutano maalum wa Baraza la Usalama siku ya Jumatano, kabla ya kuondoka kuelekea Washington ambako atapokelewa katika Ikulu ya Marekani siku ya Alhamisi. .

Zelensky anaishutumu Urusi kwa "mauaji ya halaiki" kwa kuwafukuza watoto wa Ukraine

Katika hotuba yake, Volodymyr Zelensky aliishutumu Urusi kwa "kutumia bei ya chakula (...) na nishati ya nyuklia kama silaha", akisema kwamba Moscow "haina haki ya kushikilia silaha za nyuklia", alisema kutoka kwa jukwaa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambako alishangiliwa kwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.