Pata taarifa kuu

Ukraine: Zelensky atoa wito kwa UN "kuhakikisha usalama" wa kinu cha Zaporizhia

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Alhamisi ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa "kuhakikisha usalama" wa kinu cha nyuklia cha Zaporizhia, kinachokaliwa na Urusi na kulengwa na mashambulizi kadhaa ya mabomu, huku akimpokea Katibu Mkuu Antonio Guterres.

Picha hii ya iliyotolewa na idara ya wanahabari ya rais wa Ukraine inamuonyesha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (Kulia) akiambatana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kulia) wakati wa mkutano wao mjini Kyiv, Aprili 28, 2022.
Picha hii ya iliyotolewa na idara ya wanahabari ya rais wa Ukraine inamuonyesha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (Kulia) akiambatana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kulia) wakati wa mkutano wao mjini Kyiv, Aprili 28, 2022. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Volodymyr Zelensky ameshutumu kwenye Telegram "ugaidi wa makusudi" unaochochewa na Urusi, ambao "unaweza kuwa na athari kubwa ya janga kwa ulimwengu wote". "Kwa hivyo Umoja wa Mataifa lazima uhakikishe usalama wa eneo hili la kimkakati, kupiga marufu ya silaha karibu na kinu hiki na kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi, katika eneo hilo" amebaini.

Uuzaji wa nafaka nje ya nchi unaendelea. Meli mpya imeondoka Ukraine mnamo Alhamisi Agosti 18, mamlaka ya Ukraine imetangaza. "Meli hiyo ya mizigo I MARIA imeondoka kwenye bandari ya Chornomorsk, ikiwa imesheheni tani 33,000 za mahindi. Meli ya mizigo iko njiani kuelekea Afrika Kaskazini, itawasili Misri katika siku za usoni", mamlaka ya bandari imesema kwenye ukurasa wake wa Facebook. . Jumla ya meli 25 zilizobeba bidhaa za Ukraine zimeondoka kwenye bandari za Odessa, Pivdenny na Chornomorsk (kusini mwa Ukraine) tangu kusainiwa kwa makubaliano na Umoja wa Mataifa na Uturuki ambayo yamewezesha kuondoa vikwazo vya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.