Pata taarifa kuu

Ukraine yaendelea na mashambulizi yake Kusini, Urusi yashambulia kwa mabomu Kharkiv

Mashambulizi ya Urusi yameongezeka kaskazini mashariki mwa Ukraine tangu Jumatano jioni Agosti 17 na yanaendelea Alhamisi Agosti 18, hasa huko Kharkiv: angalau watu wanne wameuawa na ishirini kujeruhiwa Alhamisi asubuhi, baada ya watu saba kuawa jioni, kulingana na vyanzo kutoka Ukraine. 

Maafisa wa kikosi cha zima moto wanafanya kazi kwenye vifusi vya jengo la makazi lililolengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi, huko Kharkiv, mnamo Agosti 17, 2022.
Maafisa wa kikosi cha zima moto wanafanya kazi kwenye vifusi vya jengo la makazi lililolengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi, huko Kharkiv, mnamo Agosti 17, 2022. © Vitalii Hnidyi / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo pia yamelenga maeneo ya Belgorod na Krasnograd karibu na mji wa pili wa nchi hiyo. Lakini Kusini, Ukraine inaendelea na mashambulizi makubwa dhidi ya vikosi vya Urusi, na kuviweka katika hali ngumu.

Vkosi vya Ukraine vimeshambulia kambi ya kijeshi huko Nova Kakhovka, karibu na mji wa Kherson: miundombinu imeharibiwa na shambulio hilo limeua askari 12 wa Urusi, makao makuu ya jeshi la Ukraine yametangaza.

Mlipuko mkali

Upande wa kusini, katika eneo linalokaliwa na Urusi, meya wa Melitopol anaripoti mlipuko mkubwa uliosikika karibu na kituo cha operesheni cha Urusi katikati mwa jiji.

Upande wa kusini unakabiliwa na mvutano mkubwa na baada ya mashambulizi ya hivi majuzi huko Crimea, ambayo yaliathiri hasa viwanja vya ndege. Moscow inapanga upya vikosi vyake, jeshi la Urusi limekimbiza ndege na helikopta zake kuisikojulikana: kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Ukraine, wavamizi wanarudisha nyuma ndege zao mbali zaidi katika eneo la shirikisho la Urusi Urusi.

Kamanda Mpya

Kremlin pia imemteua kamanda mpya mkuu wa kikosi cha baharini katika Bahari Nyeusi, Admiral Viktor Sokolov. Kikosi hicho cha kifahari cha Urusi kimekabiliwa na vikwazo vikubwa tangu kuanza kwa uvamizi, ikiwa ni pamoja na kuzama kwa meli ya Moskva mwezi wa Aprili.

Na kabla ya ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huko Lviv leo, mshauri wa masuala ya kijeshi wa Volodymyr Zelensky amesema mzozo huo, katika nyanja ya kimkakati, uko katika hali mbaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.