Pata taarifa kuu

Ukraine: Meli ya kwanza ya Umoja wa Mataifa iliyosheheni nafaka yaelekea Ethiopia

Meli ya kwanza iliyokodishwa na Umoja wa Mataifa kusafirisha nafaka ya Ukraine imeondoka kwenye bandari ya Pivdenny kusini mwa Ukraine siku ya Jumanne (tarehe 16 Agosti) ikiwa na tani 23,000 kenda Afrika, Wizara ya miundombinu ya Ukraine imetangaza.

Meli ya kwanza ya MV iliyokodishwa na Umoja wa Mataifa inapakia zaidi ya tani 23,000 za nafaka kusafirisha hadi Ethiopia, huko Yuzhne, mashariki mwa Odessa kwenye pwani ya Bahari Nyeusi, mnamo Agosti 14, 2022.
Meli ya kwanza ya MV iliyokodishwa na Umoja wa Mataifa inapakia zaidi ya tani 23,000 za nafaka kusafirisha hadi Ethiopia, huko Yuzhne, mashariki mwa Odessa kwenye pwani ya Bahari Nyeusi, mnamo Agosti 14, 2022. AFP - OLEKSANDR GIMANOV
Matangazo ya kibiashara

"Meli ya Brave Commander yenye nafaka kwa Afrika imeondoka kwenye bandari ya Pivdenny. Asubuhi ya leo, meli ya mizigo iliondoka kuelekea bandari ya Djibouti, ambako msaada wa chakula utatoewa kwa walengwa nchini Ethiopia baada ya kuwasili,” wizara imesema kwenye Telegram.

Kulingana na Wizara ya miundombinu ya Ukraine, "tani 23,000 za ngano ziko kwenye meli hii iliyokodishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani".

Akiwa katika bandari ya Pivdenny siku ya Jumapili, Waziri wa Miundombinu wa Ukraine Oleksandr Kubrakov alisema anatumai kwamba meli zingine "mbili au tatu"  zilizokodishwa na Umoja wa Mataifa zinaweza kuondoka hivi karibuni.

Hii ni shehena ya kwanza ya msaada wa chakula kuondoka Ukraine tangu makubaliano yaliotiwa saini Julai na Kyiv na Moscow, kupitia upatanishi wa Uturuki na chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, juu ya usafirishaji wa nafaka za Ukraine, kuzuiwa kwa sababu ya vita kati ya nchi hizo mbili.

Meli ya kwanza ya kibiashara iliondoka tarehe 1 Agosti, na zaidi ya meli 15 kwa jumla zimeondoka Ukraine tangu makubaliano hayo kuanza kutumika, kulingana na hesabu za mamlaka ya Ukraine, lakini hakuna meli ya Umoja wa Mataifa iliyosheheni msaada wa kibinadamu ilikuwa bado imeanza safari.

Ukraine na Urusi ni miongoni mwa wauzaji wakubwa wa nafaka duniani, ambazo zimeshuhudia kupanda kwa bei tangu kuanza kwa vita.

Kulingana na shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), rekodi ya watu milioni 345 katika nchi 82 sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, wakati hadi watu milioni 50 katika nchi 45 wako katika hatari ya njaa kama hakuna msaada wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.