Pata taarifa kuu

Guterres: Shambulio lolote dhidi ya vinu vya nyuklia ni maangamizi makubwa

Mwishoni mwa wiki hii, kinu cha nyuklia cha Zaporizhia nchini Ukraine kwa mara nyingine kulikumbwa na mashambulizi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alielezea Jumatatu kama "maangamizi makubwa" kwa shambulio lolote dhidi ya vinu vya nyuklia na kutoa wito wa kusitishwa kwa operesheni za kijeshi karibu na Zaporizhia, ili Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) liweze kufika katika eneo hilo.

Kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhia kinashikiliwa na Urusi tangu Mei 1, 2022. Picha hii ilipigwa wakati wa safari ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi mwezi Julai.
Kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhia kinashikiliwa na Urusi tangu Mei 1, 2022. Picha hii ilipigwa wakati wa safari ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi mwezi Julai. AP
Matangazo ya kibiashara

"Shambulio lolote kwenye vinu vya nyuklia ni jambo kama kujiangamaza," Antonio Guterres amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Tokyo. Ziara kama sehemu ya ukumbusho wa shambulio la nyuklia la Marekani dhidi Japan mnamo mwezi wa Agosti 1945.

Hakuna mtu, nasema nikisisitiza kwamba hakuna mtu anayeweza kukubali wazo kwamba vita vingine vya nyuklia vinaweza kutokea.

Antonio Guerres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebaini: "Tuko katika wakati ambapo hatari ya makabiliano ya nyuklia imerejea"

Kwa siku kadhaa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekuwa akionya juu ya hatari za nyuklia kwa wanadamu, akibaini kwamba yote yanasababishwa na "kutokuelewana" au "kosa la uamuzi" kutokana na "maangamizi ya nyuklia", alionya mnamo Agosti 1 katika hotuba yake huko New York. Mnamo tarehe 6 Agosti, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 77 ya shambulio la bomu la atomiki la Hiroshima, alisema binadamu alichezea "bunduki iliyojaa risasi" katika muktadha wa migogoro ya sasa inayohusiana na nyuklia.

Mashambulizi ya mabomu wikendi hii

Chini Ukraine, kituo cha kuzalisha umeme cha Zaporijia kililengwa tena na mashambulizi siku ya Ijumaa na Jumamosi, Urusi na Ukraine wakishutumiana kwa mashambulizi haya ya mabomu. Mamlaka ya Urusi inayokalia jiji la Energodar, ambako kiwanda hicho kinapatikana, ilithibitisha kwamba jeshi la Ukraine lilikuwa limerusha kifaa cha kulipuka kiitwacho "Hurricane multiple rocket launcher" usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili. "Roketi ilianguka mita 400 kutoka kwa kinu kinachofanya kazi," Urusi iliendelea, na kuongeza kuwa shambulio hilo "liliharibu" majengo ya utawala na kupiga "eneo linalotumika kwa kuhifadhi mafuta ya nyuklia." .

Wakati huo huo, kampuni ya serikali ya Ukraine Energoatom ilitangaza kwamba mmoja wa wafanyakazi kwenye kituo hiki alilazimika kulazwa hospitalini kwa "majeraha yaliyosababishwa na mlipuko " wa roketi moja iliyorushwa na Urusi Jumamosi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.