Pata taarifa kuu

Putin aishutumu Marekani kwa kuchochea mzozo wa Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumanne ameishutumu Marekani kwa kuchelewesha mzozo wa Ukraine, ambao ulianza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Moscow karibu miezi sita iliyopita, wakati tukio jipya lilipotokea katika kambi ya Urusi huko Crimea.

Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Rais wa Urusi Vladimir Putin. © MIKHAIL KLIMENTYEV, SPUTNIK VIA AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, meli ya kibinadamu inayosafirisha nafaka kwenda Afrika imeondoka Ukraine siku ya Jumanne: ikiwa ni meli ya kwanza tangu kusainiwa kwa makubaliano ya usafirishaji wa nafaka ya Ukraine mnamo mwezi Julai kati ya Kyiv na Moscow, chini ya upatanishi wa Uturuki na chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa.

Vita hivyo vilivyoanza Februari 24, vimesababisha vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Urusi na misaada ya kihistoria ya kifedha na kijeshi kwa Ukraine, na kusababisha mvutano usio na kifani, hasa kati ya Washington na Moscow.

Vladimir Putin ameikosoa Marekani kwa kutaka "kuyumbisha usalama" wa dunia, pia akitoa mfano wa ziara ya hivi majuzi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi huko Taiwan.

"Hali ya Ukraine inaonyesha kwamba Marekani inajaribu kuchochea mzozo huu. Na inafanya vivyo hivyo kwa kukuza uwezekano wa mzozo barani Asia, Afrika, Amerika Kusini," Putin amehutubia Mkutano wa Kimataifa wa Usalama huko Moscow.

Tuhuma hizo zinakuja wakati kambi za kijeshi za Urusi katika rasi ya Crimea iliyotwaliwa na Urusi mwaka 2014, ambayo ni inatumiwa kwa kusaidia vikosi vya  Urusi, ikikumbwa na mashambulizi makubwa ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.