Pata taarifa kuu

Ukraine: Guterres, Erdogan na Zelensky wakutana Lviv na kujadili mtambo wa Zaporizhia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wanatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Lviv, magharibi mwa Ukraine, Alhamisi Agosti 18

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kupongeza mkataba wa mauzo ya nafaka huko Lviv. Hapa, ilikuwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo, huko Istanbul, Julai 22, 2022.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kupongeza mkataba wa mauzo ya nafaka huko Lviv. Hapa, ilikuwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo, huko Istanbul, Julai 22, 2022. © Umit Bektas / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Wakati wa mkutano huu, mauzo ya nafaka ya Ukraine yatajadiliwa, lakini pia hali katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhia, kinachidhibitiwa kwa sasa na jeshi la Urusi na kulengwa kwa mashambulizi ya anga. Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, inataka ukaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, lakini hili linawezekana tu ikiwa Moscow itatoa idhini yake.

Ni mkutano wenye changamoto nyingi ambao utafanyika katika jiji la Lviv, magharibi mwa Ukraine.

Iwapo makubaliano ya Julai 22 kuhusu mauzo ya nafaka yaliyotiwa saini mjini Istanbul kati ya Moscow na Kyiv, chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa na Uturuki, hayajanyamazisha ghasia nchini Ukraine, hata hivyo yamewezesha kuondoka kwa meli 25 zilizosheheni vyakula kupitia bandari tatu za Ukraine.

Katika mji wa Yuzhne, kusini mwa nchi hiyo, meli ya kwanza ya msaada wa kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, iliyosheheni tani 23,000 za ngano, iliweza kuondoka Jumanne Agosti 16 kuelekea Pembe ya Afrika.

Wakati mavuno yameanza nchini Ukraine, mamilioni ya tani za nafaka bado zimehifadhiwa katika mamia ya maghala kote nchini.

Meli tano zaidi za nafaka zinatarajiwa

Mamlaka ya Ukraine ilitangaza Jumatano Agosti 17 kwamba walikuwa wakitarajia meli nyingine tano katika bandari ya Chornomorsk. Ikiwa na zaidi ya tani 70,000 za bidhaa za kilimo, utakuwa msafara mkubwa zaidi kushuhudiwa tangu makubaliano.

Waziri wa miundombinu wa Ukraine anatumai kuwa kwa kiwango hiki watakaribia kiasi cha tani milioni tano kwa mwezi kilichokuwa kikipatikana kabla ya vita.

Ni katika bandari ya kwanza ya Ukraine, Odessa, ambapo viongozi hao watatu watakwenda kujionea wenyewe uwezo wa kifaa hicho Ijumaa, Agosti 19. Kabla ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenda Istanbul siku ya Jumamosi kutembelea kituo cha uratibu ambapo wawakilishi wa Ukraine, Urusi, pamoja na Uturuki na Umoja wa Mataifa wapo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.