Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Kundi la Wagner ladai kuteka sehemu ya mashariki ya Bakhmut

Kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner linadai Jumatano hii, Machi 8 kudhibiti sehemu ya mashariki ya mji wa Bakhmut, kitovu cha mapigano ya umwagaji damu kwa miezi kadhaa na kuanguka kwake kutachangia kwa jeshi la Urusi kusonga mbele mashariki mwa Ukraine, kulingana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. 

Mwanajeshi wa Ukraine karibu na Bakhmut, katika jimbo la Donetsk, Ukraine, Jumanne, Machi 7, 2023.
Mwanajeshi wa Ukraine karibu na Bakhmut, katika jimbo la Donetsk, Ukraine, Jumanne, Machi 7, 2023. AP - Libkos
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Bakhmut unaweza kuanguka "katika siku chache zijazo", ameonya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za kujihami za Magharibi, NATO, siku ya Jumatano.

"Vikosi vya Wagner vimechukua sehemu nzima ya mashariki ya Bakhmut, maeneo yote ambayo ni mashariki mwa Mto Bakhmutka" unaopita katika jiji hili, amesema mkuu wa kundi hili la mamluki wa Urusi, Evguéni Prigojine.

Katika ripoti yake ya hivi punde, iliyochapishwa Jumanne Machi 7, Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW), kundi la wataalam wa Marekani, lilibaini kwamba wanajeshi wa Kremlin "huenda" waliteka sehemu hii ya mashariki, baada ya "jeshi la Ukraine kujiondoa" katika eneo hilo. Kulingana na shirika la habari la AFP, halijaweza kuthibitisha taarifa hizi kutoka kwa chanzo huru.

Kwa upande wake, Volodymyr Zelensky amehakikisha kwamba wanajeshi wake wameazimia kuushikilia mji huo, katika mahojiano na televisheni ya Marekani ya CNN yaliyorushwa leo Jumatano. "Nilifanya kikao na mkuu wa majeshi jana na makamanda wakuu wa jeshi...na wote walisema itabidi tuwe imara huko Bakhmut," amesema. "Kwa kweli, tunapaswa kufikiria juu ya maisha ya askari wetu. Lakini lazima tufanye kila tuwezalo huku tukipokea silaha, vifaa na jeshi letu likijiandaa kukabiliana na mashambulizi hayo,” ameongeza. Baada ya Bakhmut, Warusi "wataweza kwenda mbali zaidi. Wataweza kwenda Kramatorsk, Sloviansk, ikiwa njia itakuwa huru" kwao "kuelekea miji mingine ya Ukraine", ameonya rais wa Ukraine.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.