Pata taarifa kuu

Wagner yaishtumu Urusi kwa kutoipa silaha zaidi

NAIROBI – Kiongozi wa kundi la wapiganaji binafsi nchini Urusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, anasema wapiganaji wake hawapati silaha za kutosha kutoka kwa serikali ya Moscow, ili kuendelea kupambana katika mji wa Bakhmut, Mashariki mwa Ukraine.

Mkuu wa mamluki wa Wagner nchini Urusi, Yevgeny Prigozhin.
Mkuu wa mamluki wa Wagner nchini Urusi, Yevgeny Prigozhin. via REUTERS - CONCORD PRESS SERVICE
Matangazo ya kibiashara

Mshirika huyo wa karibu wa rais Vladimir Putin, anaonya kuwa huenda wasifanikiwe kwenye mji wa Bakhmut, kwa kutopata silaha inazohitaji, suala ambalo anasema huenda ni usaliti.

Yevgeny, ameongeza kuwa iwapo wapiganaji wake watajiondoa Bakhmut, êneo lote litakuwa mikononi mwa vikosi vya Ukraine, katika mji ambao Urusi inasema ni ardhi yake, baada ya kuchukua jimbo la Donetsk, mwaka uliopita kwa kuandaa kura ya maoni.

Kwa miezi kadhaa sasa, kundi la Wagner linaloshirikiana kwa karibu na wanajeshi wa Urusi, wamekuwa wakipambana kuudhibiti mji wa Bakhmut, na sasa kiongozi huyo anailaumu Wizara ya Ulinzi kwa kuchelewesha, upatikanaji wa silaha.

Licha ya makabiliano makali ambayo yamekuwa yakiendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja, ambacho Urusi imeivamia Ukraine, wachambuzi wa mzozo huu wanasema, udhibiti wa mji huo hauna umuhimu mkubwa wa kimkakati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.