Pata taarifa kuu

Ukraine: jeshi lafikia 'makubaliano' 'kuendelea kulinda Bakhmout'

Kuna "makubaliano" ndani ya jeshi la Ukraine 'kuendelea kulinda' na 'kutetea' Bakhmout, kitovu cha mapigano mashariki, licha ya hatari ya kuzingirwa na wanajeshi wa Urusi, mshauri wa rais wa Ukraine amesema siku ya Jumatatu.

Wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kupambana dhidi ya Urusi huko Bakhmut.
Wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kupambana dhidi ya Urusi huko Bakhmut. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Kuna maafikiano kati ya wanajeshi juu ya hitaji la kuendelea kuulinda mji na kuvimaliza vikosi vya adui, huku wakijenga safu mpya za ulinzi sambamba iwapo hali itabadilika," amesema Mykhaïlo Podoliak, akibaini kwamba wanajeshi wa Ukraine hawataongoka katika mji wa Bakhmut.

Amesema, "ulinzi wa Bakhmut ulifanikisha malengo yake" kwa kuchosha vikosi vya Urusi kutoa wakati kwa jeshi la Ukraine kwa kutoa mafunzo kwa "makumi ya maelfu ya wanajeshi kutayarisha kuanzisha mashambulizi makubwa ".

"Hata kama viongozi wa kijeshi wataamua wakati fulani kurejea kwenye nafasi zenye manufaa zaidi, ulinzi wa Bakhmout utakuwa wa mafanikio makubwa ya kimkakati," almeema Mykhaïlo Podoliak.

Maendeleo ya vikosi vya Urusi

Walakini, alisema kuwa hakuna uamuzi wowote juu ya uwezekano wa kujiondoa kwa Ukraine  umechukuliwa kwa wakati huu.

Kinyume chake, makao makuu ya jeshi la Ukraine yalitangaza Jumatatu nia yake ya "kuimarisha" misimamo yake huko Bakhmut, ambapo pande zote mbili zimepata hasara kubwa katika miezi ya hivi karibuni.

Wanajeshi wa Urusi wamesonga mbele katika wiki za hivi karibuni kaskazini na kusini mwa mji huo, na kukata njia tatu kati ya nne za zinazotumiwa kwa kusafirisha chakula nchini Ukraine na kuacha moja tu inayoelekea magharibi zaidi kuelekea Chassiv Iar kama njia ya kutokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.