Pata taarifa kuu

Ikulu ya rais wa Ukraine: Jeshi la Ukraine linataka 'kuimarisha' ngome zake Bakhmut

Jeshi la Ukraine linapanga "kuimarisha" ngome zake huko Bakhmut, kitovu cha mapigano na wanajeshi wa Urusi mashariki mwa nchi, ikulu ya rais wa Ukraine imesema leo Jumatatu baada ya  uvumi kuhusu kujiondoa kwa wanajeshi wa Ukraine katika eneo hili, shirika la habari la AFP limeandika.

Wanajeshi wa Ukraine wakiendelea kukabilianana mashambulizi ya urusi huko Bakhmut.
Wanajeshi wa Ukraine wakiendelea kukabilianana mashambulizi ya urusi huko Bakhmut. AFP - ARIS MESSINIS
Matangazo ya kibiashara

Urusi imekuwa ikitafuta kudhibiti mji wa Bakhmut tangu msimu wa joto wa mwaka 2022, mji ulioko mashariki mwa Ukraine ambao ulikuwa na wakazi karibu 70,000 kabla ya uvamizi wa Urusi uliozinduliwa mwaka mmoja uliopita.

Vita "mbaya na ngumu". Katika tamko lake la kila siku, siku ya Jumapili, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisifu "ushujaa" wa askari wanaopambana na jeshi la Urusi katika mkoa wa Donbass, mashariki mwa nchi, ambapo mji wa Bakhmut unapatikana, ambao umekuwa 'kitovu cha vita kamili, na kutishiwakuzinirwa a wanajeshi wa Urusi. Rais wa Ukraine alisema ni kiasi gani vita hii imesababisha hasara nzito na kubwa kwa pande zote kwa miezi kadhaa.

 Wakati huo huo kwa agizo la Rais Zelensky lililochapishwa Jumatatu asubuhi, Jenerali Oleksandr Oleksiyovych ameteuliwa Kamanda mkuu wa jeshi. Alikuwa kabla ya uteuzi huu akihudumu kama Makamu wa Waziri wa Ulinzi wa Ukraine.

  'Zaidi ya mashambulizi 130 ya adui' yalirudishwa nyuma katika kipindi cha saa 24

Wakati wanajeshi wa Urusi wanaendelea na juhudi zao za kuzingira jiji la Bakhmut, makao makuu ya jeshi la Ukraine limesema kwamba "zaidi ya mashambulio ya adui 130" yalishtushwa katika masaa 24 iliyopita, katika katika maeneo kadhaa ya vita, hasa huko Kopiansk, Lyman, Bakhmout na Avdiïvka.

  Jiji la Zaporijjia laomboleza msiba wa siku moja. Baada ya watu kumi na tatu kuuawa katika bomu lililolenga jengo la makazi mnamo Machi 2, meya wa Zaporijjia aliamua kutangaza siku hii ya Jumatatu kuwa siku ya maombolezo. "Ni huzuni mkubwa, anaandika Anatolii Kurtiev kwenye Telegraph. Kwa pamoja, wacha tutowe heshima za mwisho kwa wale wote ambao waliuawa wakati usiku wa Machi 2."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.