Pata taarifa kuu

Urusi: Putin aagiza usalama kuimarishwa mipakani

NAIROBI – Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza maafisa wake wa usalama kuimarisha ulinzi zaidi katika mpaka wake na Ukraine, kufuatia kuanguka kwa ndege isiyokuwa na rubani katika ardhi yake.

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameagiza usalama kuimarishwa katika mipaka yake
Rais wa Urusi Vladmir Putin ameagiza usalama kuimarishwa katika mipaka yake © AP / Pavel Bednyakov
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo isiyokuwa na rubani, ilianguka Kilomita 100 Kusini Mashariki mwa jiji kuu Moscow, huku nyingine ikiangushwa Kusini mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa Wiza ya Ulinzi.

Moscow inadai kuwa ndege hiyo ililenga kuwashambulia raia na kuharibu miundo mbinu katika ardhi yake, katika jimbo la Kolomna na zilikuwa zimetokea nchini Ukraine.

Hata hivyo, Ukraine inasema haikutuma ndege zake katika ardhi ya Urusi.

Wakati hayo yakijiri, Ukraine inasema wanajeshi wake wanaendelea kupambana katika mji wa Bakhmut, Mashariki mwa nchi hiyo, dhidi ya vikosi vya Urusi vinavyotaka kudhibiti mji huo na hali inasalia kuwa ya wasiwasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.