Pata taarifa kuu

Zelensky kupambana na Urusi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kulihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo Jumatano, akikabiliana na Urusi mwanachama wa kudumu kwa mara ya kwanza tangu vita kuanza.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 19, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 19, 2023. © TIMOTHY A. CLARY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ukiwa unaendelea, rais wa Ukraine anaendelea na mashambulizi yake ya kidiplomasia huko New York ambako viongozi wakuu wa dunia wamekusanyika, rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wakiwa hawakushiriki katika vikao hivi.

Volodymyr Zelensky atakuwa miongoni mwa wa kwanza kuzungumza wakati wa mkutano huu maalum, uliodhibitiwa kwa uangalifu, ambapo zaidi ya viongozi sitini wamepangwa kutoa hotuba zao chini ya uenyekiti wa Albania, kulingana na ajenda iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Mkutano huo unafanyika kwa kiwango cha juu na viongozi wengi wanatarajiwa kuzungumza.

Hii ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini mwake, Februari 24, 2022, kwa rais Zelensky kuzungumza ana kwa ana mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, chombo ambacho zaidi ya hayo kimezorota wakati huu kufuatia kura ya turufu ya Urusi.

Urusi, kwa hakika, itawakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov ambaye aliwasili Jumanne jioni huko New York, katika kiwango sawa na Marekani na Ufaransa na Antony Blinken na Catherine Colonna mtawalia.

Haijabainika iwapo Bw. Lavrov atahudhuria hotuba ya Rais Zelensky ana kwa ana au atawakilishwa wakati wa hotuba yake, kama ilivyokuwa wakati wa mkutano wa Baraza Kuu katika ngazi ya wakuu wa diplomasia.

Kando na Marekani, hakuna mjumbe mwingine wa kudumu wa Baraza la Usalama anayewakilishwa katika ngazi ya juu zaidi katika kikao hiki cha kidiplomasia cha kila mwaka ambayo ni Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na ambalo linaanza siku yake ya pili Jumatano. Ukosefu ambao baadhi ya wanadiplomasia wanaona kuwa ni ishara mbaya kwa Umoja wa Mataifa.

Siku hiyo pia itakuwa kali na mkutano wa pande mbili unaotarajiwa kati ya Rais Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, kando ya Baraza Kuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.