Pata taarifa kuu

Vifaru Ukraine: Poland yamweka Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz chini ya shinikizo

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki leo Jumatatu Januari 23 kwamba nchi yake itaomba makubaliano ya Berlin ili kuipa Ukraine vifaru vya Leopard vilivyotengenezwa nchini Ujerumani.

Kifaru Leopard 2, wakati wa maonyesho ya Eurosatory 2010 huko Villepinte, Ufaransa.
Kifaru Leopard 2, wakati wa maonyesho ya Eurosatory 2010 huko Villepinte, Ufaransa. ERIC PIERMONT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujerumani "haitapinga" nia ya Poland ya kupelekea Ukraine vifaru vya Leopard, ambavyo inaviomba ikisisitiza, mkuu wa diplomasia ya Ujerumani, Annalena Baerbock, alitangaza Jumapili Januari 22 kwenye kituo cha televisheni cha Ufaransa LCI. Kwa hivyo anaweka shinikizo kwa Kansela Scholz, ambaye amejionyesha kuwa na wasiwasi zaidi juu ya suala hilo.

"Ikiwa tutaulizwa swali, hatutapinga" kuipa kyiv vifaru hivi vilivyotengenezwa na Ujerumani, ametangaza waziri wa mazingira, ambaye anatawala kwa muungano pamoja na wanademokrasia wa kijamii wa Olaf Scholz na waliberali, wakati wa mahojiano na kituo cha rungina cha LCI.

Uamuzi wa mwisho, hata hivyo, ni wa Kansela Olaf Scholz, ambaye hadi sasa amekataa kutoa maoni juu ya suala la utoaji wa njia hizi zisizo za moja kwa moja, kama tu lile la kusambaza vifaru vya Leopards moja kwa moja kutoka kwa hisa za Ujerumani. Kansela, jana huko Paris, hakuwa na utata zaidi, akihakikishia hata hivyo kwamba "Ukraine lazima ijue kwamba tutaendelea kuisaidia", na kusisitiza ushirikiano wa kimataifa.

"Uamuzi [...] unategemea mambo mengi na unachukuliwa kwenye baraza la mawaziri", amesisitiza kwa upande wake Waziri mpya wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, katika mahojiano kwenye televisheni ya Ujerumani ARD, iliyotangaza muda mfupi baada ya mahojiano na mkuu huyo wa diplomasia. Bw. Pistorius, Mwanademokrasia wa Kijamii kama Kansela Scholz, hata hivyo hakuhojiwa kuhusu matamshi ya Bi. Baerbock.

Shinikizo kutoka Poland na Mataifa ya Baltic

Siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki alijitokeza kwa mara nyingine tena, akilaani hatu ya Berlin kukataa kuipa Kyiv vifaru vikubwa"kutokubalika". Poland na Ufini wamejitolea kupeleka vifaru vya Leopards ambavyo wanamiliki, lakini wanahitaji idhini rasmi kutoka Berlin kwa mauzo ya nje tena. Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tatu za Baltic waliita siku moja kabla, siku ya Jumamosi, Ujerumani kuipa Ukraine "mara moja" vifaru vya Leopard  ili kuisaidia kukomesha uvamizi wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.