Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-USALAMA

Ghasia nchini Ufaransa: Emmanuel Macron aahirisha ziara yake ya serikali nchini Ujerumani

Baada ya siku nne za ghasia nchini Ufaransa zinazohusishwa na kifo cha kijana Nahel, rais wa Ufaransa ameomba kuahirishwa kwa ziara yake ya kiserikali iliyopangwa kufanyika Jumapili huko Outre-Rhin hadi tarehe ambayo itakayotangazwa baadaye.

Emmanuel Macron mnamo Juni 23, 2023 huko Paris.
Emmanuel Macron mnamo Juni 23, 2023 huko Paris. AFP - LEWIS JOLY
Matangazo ya kibiashara

"Rais wa Jamhuri na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier walizungumza Jumamosi hii, Julai 1, 2023. Kwa kuzingatia hali ya nchi, Rais wa Jamhuri amebaini kwamba angependelea kubaki Ufaransa kwa siku chache zijazo", imebaini Elysée.

"Rais wa Ujerumani anasikitishwa na kuahirishwa kwa ziara hiyo na anaelewa kikamilifu kwa sababu ya hali" nchini Ufaransa, ikulu ya rais wa Ujerumani imesema katika taarifa. Frank-Walter Steinmeier “anafuatilia hali nchini Ufaransa kwa umakini mkubwa. Anatumai kuwa ghasia mitaani zitakoma hivi karibuni na kwamba amani ya kijamii inaweza kurejeshwa tena,” ikulu ya rais wa Ujerumani imeongeza.

Kwa mujibu wa wasaidizi wa rais wa Ufaransa, hakuna tarehe mpya iliyopangwa. Huko Paris, chanzo kimoja kinasisitiza kwamba maafisa wa Ufaransa na Ujerumani wana fursa nyingi za kukutana, na kwamba ziara ya serikali ni njia kuu ya kusherehekea urafiki wa Ufaransa na Ujerumani, zaidi ya mkutano wa kisiasa.

Mwishoni mwa mwezi Machi, ziara ya serikali ya Mfalme Charles III nchini Ufaransa iliahirishwa kutokana na mzozo wa kijamii uliohusishwa na mageuzi ya pensheni.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.