Pata taarifa kuu

Kifo cha Nahel: Mivutano yaripotiwa katika miji mingi nchini Ufaransa, vikosi vya usalama vyatumwa

Baada ya siku mbili za vurugu ambazo zimeongezeka kwa kasi, hali inatarajia kuwa mbaya zaidi kulingana na taarifa ya upelekezi. Kuna hatari vikosi vya usalama na majengo ya serikali kulengwa katika vurugu hizi, kulingana na taarifa hiyo.

Magari kadhaa yalichomwa moto huko Nanterre kando ya maandamano meupe baada ya kifo cha kijana Nahel mnamo Juni 29.
Magari kadhaa yalichomwa moto huko Nanterre kando ya maandamano meupe baada ya kifo cha kijana Nahel mnamo Juni 29. AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Alasiri, maandamano meupe ya kutoa heshima kwa Nahel yalileta pamoja watu 6,200 huko Nanterre. Lakini maandamano hayo yalimalizika kwa hali ya sintofahamu, na makabiliano, huku kukirushwa mabomu ya machozi na fataki, visa vya moto vimeripotiwa na uharibifu wa mali majengo ya serikali.

Wakai huo huo watu 150 wamekamatwa baada ya mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika jiji la Paris. Ghasia hizo zimezuka baada ya polisi kumpiga risasi na kumuua kijana mmoja wa miaka 17 mwenye asili ya Afrika Kaskazini.

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji na ghasia za kuchoma moto magari, na vitu vingine zilitokea kwenye kitongoji cha Nanterre na kwenye maeneo mengine ya magharibi ya mji wa Paris. Ghasia hizo pia zimeenea katika miji mingine. Kutokana na hali hiyo ya machafuko maalfu ya maafisa wa polisi wamepelekwa ili kuzima ghasia hizo. Wizara ya mambo ya ndani imesema maafisa wa polisi 2,000 wamepelekwa kukabiliana na hali ya mjini Paris na miongoni mwao kadhaa wamejeruhiwa baada ya mapambano na waandamanaji wenye hasira.

Mauaji ya Nahel kwenye ukaguzi wa trafiki yaliyonaswa kwenye video, yaliishtua nchi na kuchochea mvutano wa muda mrefu kati ya polisi na vijana wanaoishi kwenye makazi yaliyo katika vitongoji vya watu wenye maisha duni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.