Pata taarifa kuu

Kifo cha Nahel: Mbappé na wachezaji wa timu ya soka ya Ufaransa wapandwa na hasira

Kifo cha Nahel, kijana mwenye umri wa miaka 17, na mazingira yake kwa kurushwa hewani video ya tamthilia hiyo kwenye mitandao ya kijamii imeibua hisia na hasira zinazoongezeka tangu siku ya Jumanne. Wanariadha kadhaa na hasa wanasoka kutoka timu ya soka ya Ufaransa wamekosoa tabia ya baadhi ya maafisa wa polisi.

Kylian Mbappé na Aurélien Tchouaméni, wanalaani kifo cha Nahel.
Kylian Mbappé na Aurélien Tchouaméni, wanalaani kifo cha Nahel. AFP - THOMAS COEX
Matangazo ya kibiashara

"Ninajisikia vibaya kwa nchi yangu, Ufaransa. Ni hali isiyokubalika! ameandika Kylian Mbappé na wafuasi wake milioni 12 kwenye Twitter. Jules Kounde, beki wa timu ya Ufaransa, amelaani "kitendo cha kikatili la afisa wa polisi aliyehusika na tukio hilo". Mike Maignan, kipa wa The Blues na AC Milan, anashangaa: “Risasi kichwani. Siku zote ni kwa watu wale wale, kuwa katika makosa hupelekea kifo”.

Kwa upande wake Ryan Cherki, aliyefunga bao Jumatano jioni akiichezea timu ya soka ya Ufaransa  amesema ("Kila mtu anajua kilichotokea"), wachezaji wenye asili ya wahamiaji ambao wengi wao waliishi katika maeneo yenye maisha magumu, wameghadhabihwa na tukio hili. Hisia zao ni kwamba watu wote wako sawa katika majibu ya vikosi vya usalama.

Aurélien Tchouaméni, kiungo wa kati wa Real Madrid, amechapisha barua ndefu kwenye mitandao ya kijamii. "Nahel angekuwa mdogo wangu, ningependa kuelewa kwa nini kisa kinaonekana kuwa kizito sana linapokuja suala la aina fulani ya mtu. Elewa kwa nini ilibidi video itoke ili kesi isifunikwe. "

Baada ya kifo cha Nahel siku ya Jumanne huko Nanterre, kwa usiku wa pili mfululizo, makabiliano na ghasia zilizuka huko Nanterre, lakini pia, usiku wa Jumatano kuamkia siku ya Alhamisi, katika miji mingine ya Ufaransa. Visa vya moto na uharibifu kadhaa wa mali ya umma vimeripotiwa. Watu mia moja na hamsini walikamatwa. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameshutumu leo Alhamisi asubuhi "matukio yasiyofaa ya ya vurugu dhidi ya taasisi na Jamhuri".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.