Pata taarifa kuu

Kijana aliyeuawa na afisa wa polisi Ufaransa: 'Haielezeki' na 'haisameheki', asema Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Jumatano ametaja kitendo cha afisa wa polisi kumuua kwa risasi kijana mmoja kuwa 'hakielezeki' na 'hakisameheki'.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

 

Kijana mwenye umri wa miaka 17 aliuawa na afisa wa polisi siku moja kabla karibu na Paris, baada ya kukataa kutii amri ya afisa polisi aliyemtaka asimishe gari lake ili liweze kukaguliwa.

"Hakuna, hakuna kinachohalalisha kifo cha kijana huyu", amesema rais wa Ufaransa, akitaja "hisia za taifa zima" na kuonyesha "heshima na mapenzi (yake) kwa familia ya mhanga.

"Tuna kijana ambaye aliuawa, kitendo ambacho hakielezeki, hakisameheki na kwanza kabisa haya ni maneno ya upendo, maumivu ya pamoja na msaada kwa familia yake na wapendwa wake," Emmanuel Macron amewaambia waandishi wa habari.

Nahel M.,17, aliuawa baada ya kukataa kutii amri ya afisa polisi aliyemtaka asimishe gari lake ili liweze kukaguliwa huko Nanterre, magharibi mwa mji mkuu. Afisa aliyefyatua risasi yuko chini ya ulinzi.

Kwa mujibu wa rais wa Ufaransa, polisi inaundwa na "wanawake na wanaume ambao pia wanatoka sehemu zote za Jamhuri na wamejitolea kutulinda na kuitumikia Jamhuri".

"Ninawashukuru kila siku kwa hilo", ameongeza, akikumbusha kwamba majukumu yao yanatekelezwa "ndani ya mfumo wa kimaadili ambao umefafanuliwa, ambao lazima uheshimiwe".

Ametaka sheria ifuate mkondo wake, ili haki itendeke.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.