Pata taarifa kuu

Ufaransa: Polisi aliyetekeleza mauaji ameomba msamaha

Nairobi – Nchini Ufaransa, kwa mara nyingine kumeshuhudiwa makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi katika miji mbalimbali, kufuatia kisa cha polisi kumpiga risasi na kumuua Nahel, kijana mwenye umri wa miaka 17 katika kizuizi cha trafiki, Magharibi mwa jiji la Paris.

Rais Macron amelaani tukio hilo suala analosema halikubaliki
Rais Macron amelaani tukio hilo suala analosema halikubaliki AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Kwa usiku wa tatu mfululizo, waandamanaji wenye hasira kwenye miji ya Marseille, Lyon, Lille na mingine, wameandamana na kuzua fujo kuonesha hasira zao, baada ya kuuawa kwa kijana huyo mwenye asili ya Algeria na Morocco.

Licha ya kutumwa kwa maafisa wa polisi zaidi ya Elfu 40 kukabiliana na waandamaji hao, waliochoma magari na maduka, huku mamia ya waandamanaji wakikamatwa.

Mama yake Nahel, amezungumza kwa mara ya kwanza na kusema anamlamu polisi aliyemuua mtoto wake na kutaka awajibishwe.

Maandamano yamefanyika katika baadhi ya maeneo nchini Ufaransa
Maandamano yamefanyika katika baadhi ya maeneo nchini Ufaransa AP - Michel Euler

Naye Polisi aliyetekeleza mauji hayo, amekamatwa na kufunguliwa mashtaka na kupitia kwa wakili wake, ameomba radhi kwa familia ya kijana huyo.

Rais Emmanuel Macron ameomba utulivu, na kulaani mauaji hayo akisema, hakuna sababu inayoweza kutolewa kutetea kilichokea.

Machafuko yanayoshuhudiwa nchini Ufaransa, yanaleta kumbukumbu ya mwaka 2005 ambapo wavulana wawili wenye asili ya Afrika waliouawa mikononi mwa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.