Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Putin ataka kuonyesha kuwa Urusi iko mikononi mwake

Rais wa Urusi, baada ya kukanusha kwa miaka mingi, hatimaye amekiri na kufafanua ufadhili wa moja kwa moja wa serikali yake kwa kundi la wanamgambo la Wagner. Pia ameonyesha kuunga mkono kwa utawala wake kwa vikosi vyote vya usalama. Huu ni ujumbe wake muhimu.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akisikiliza wimbo wa taifa kabla ya kutoa hotuba kwa vitengo vya Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Walinzi wa Kitaifa wa Urusi (Rosgvardiya), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi, Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi na kikosi cha ulinzi wa taifa, ambao walisimami utulivu na usalama wakati wa uasi, huko Kremlin, Moscow, Urusi, Jumanne, Juni 27, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akisikiliza wimbo wa taifa kabla ya kutoa hotuba kwa vitengo vya Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Walinzi wa Kitaifa wa Urusi (Rosgvardiya), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi, Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi na kikosi cha ulinzi wa taifa, ambao walisimami utulivu na usalama wakati wa uasi, huko Kremlin, Moscow, Urusi, Jumanne, Juni 27, 2023. AP - Sergei Guneyev
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow

"Tulifadhili kundi hili kikamilifu kupitia bajeti ya Wizara ya Ulinzi na bajeti ya serikali. Kuanzia mwezi Mei 2022 hadi mwezi Mei 2023 pekee, serikali ililipa mishahara ya kampuni ya Wagner na marupurupu ya rubles bilioni 86 milioni 262, ikiwa ni pamoja na pesa taslimu bilioni 70 milioni 384, marupurupu ya rubles bilioni 15 milioni 877, malipo ya bima bilioni 110 milioni 179, wakati mmiliki wa kampuni ya Concord kupitia mikataba na jeshi na (licha ya ukweli kwamba matengenezo yote ya Wagner yalitegemea serikali) alipata rubles bilioni 80 kwa kutoa chakula kwa jeshi. Serikali ilitoa msaada wa kifedha na Concord, wakati huo, ilipata bilioni 80. Natumai wakati huo hakuna mtu aliyeiba chochote au aliiba kidogo tu. Kwa kweli, hili pia tutalishughulikia, "rais wa Urusi alisema.

Kwa hivyo kazei bado ipo na haijulikani lini itamalizika na tishio sio tu kwa kundi hili wanamgambo la Wagner pekee. Kila mtu nchini Urusi anatarajia kile ambacho baadhi ya vyombo vya habari huita "mabadiliko ya kibinafsi", kumaanisha kumsaka mtu yeyote ambaye huenda alikosea kuangusha utawala wikendi iliyopita. Kwa wanajeshi waaminifu, kwa mfano kikosi cha ulinzi wa taifa kinachoongozwa na mmoja wa walinzi wake wa zamani, rais, kwa upande mwingine, ametoa taji la heshima, na uwezo kwa kikosi hiki. Kwa mara ya kwanza tangu kuundwa kwa kikosi hiki mnamo 2016, Rosgvardia - kinachoongozwa na mlinzi wa zamani wa Vladimir Putin - kitapokea mizinga na vifaa vingine vizito.

Putin awashukuru wanajeshi waliozuia 'vita vya wenyewe kwa wenyewe'

Mlolongo huu wa hatua hizi kuonyesha kwamba nchi iko mikononi mwake, Vladimir Poutine alianza Jumatatu jioni Juni 26 kwa hotuba fupi. Lakini jumbe muhimu zaidi zilitolewa Jumanne. Kuanzia FSB hadi jeshi, vikosi vyote vya usalama vilikusanywa na kusifiwa na Vladimir Putin kwa tabia zao wakati wa uasi wa Wagner.

"Katika mapigano na waasi, wenzetu, marubani, waliouawa. Hawakukurupuka na walitimiza kwa heshima wajibu wao wa kijeshi. Ninawaomba kuwakumbuka tukisalia kimya kwa dakika moja, "alisema Mkuu wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.