Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Maafisa wa usalama wa rais wa Afrika Kusini wazuiliwa nchini Poland

Maafisa wa usalama wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambao walipaswa kuandamana naye katika ujumbe wake wa upatanishi nchini Ukraine siku ya Ijumaa wamezuiliwa nchini Poland, maafisa kutoka nchi zote mbili wanasema, na hivyo kuzua tukio la kidiplomasia.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa marais 4 wa nchi za Afrika wanaokwenda Kyiv na Moscow kukutana na viongozi wa nchi hizi mbili.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa marais 4 wa nchi za Afrika wanaokwenda Kyiv na Moscow kukutana na viongozi wa nchi hizi mbili. REUTERS - ESA ALEXANDER
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa usalama wa Bw Ramaphosa, Jenerali Wally Rhoode, ameshutumu mamlaka ya Poland kwa kuwa 'ya ubaguzi wa rangi' na 'kuhatarisha' maisha ya rais wake, baada ya watu wake kuzuiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chopin huko Warsaw.

Serikali ya Poland imejibu siku ya Ijumaa kwa kuona kauli hizi "zisizofaa", ikieleza kuwa baadhi ya watu waliokuwa kwenye ndege kutoka Afrika Kusini hawakuwa na leseni ya kubeba silaha na hivyo hawakupewa idhini ya kutua.

"Hawakuruhusiwa kuondoka kwenye ndege na silaha zao. Walitakiwa kubaki ndani ya ndege," amesema afisa wa serikali katika idara maalum ya Poland, Stanislaw Zaryn.

Ndege hiyo ya kukodi iliondoka Pretoria mapema siku ya Alhamisi, ikiwa na takriban watu 120, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama vya Afrika Kusini na waandishi wa habari ambao walipaswa kumfuata Rais Ramaphosa katika ziara yake mjini Kiev kama sehemu ya ujumbe wa upatanishi wa amani unaoongozwa na viongozi wa Afrika.

Cyril Ramaphosa aliwasili katika mji mkuu wa Poland siku ya Alhamisi kwa ndege ya rais wa Afrika Kusini Inkwazi, kisha akasafiri kwa treni hadi Kyiv, ambako aliwasili siku ya Ijumaa, kulingana na ofisi ya rais.

Tukio hilo kwenye uwanja wa ndege lilimkasirisha Jenerali Rhoode, ambaye alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari bila kutarajia akiwa ndani ya ndege ya kukodi.“Wanatuchelewesha, wanaweka maisha ya rais hatarini,” amesema.Jenerali huyo katika video iliyowekwa kwenye Twitter.

“Wanasema hatuna vibali, tuna vibali,” alisema huku akikiri baadhi ya maafisa wa timu yake walikuwa na nakala za karatasi muhimu tu. "Angalia jinsi walivyo wabaguzi," amesema. Baadaye kidogo, msemaji wa Rais Ramphosa, Vincent Magwenya, ameliita tukio hilo kuwa la kusikitisha, huku akiongeza kuwa halijahatarisha usalama wa rais.

"Misheni iliyosalia inaendelea vizuri na kama ilivyopangwa," amehakikisha Bw. Magwenya kabla ya kuongeza: "Rais amefika Kyiv salama".

Maafisa wa Afrika Kusini wameanza majadiliano na wenzao wa Poland ili kuvunja mvutano huo na kuruhusu timu ya usalama na waandishi wa habari, ambao pia wamezuiliwa, kuendelea na safari yao. Ijumaa alasiri, baadhi ya waandishi wa habari waliruhusiwa kushuka baada ya zaidi ya saa 24 kwenye uwanja wa ndege.

Baada ya Kyiv, upatanishi wa Afrika lazima uende kaskazini-magharibi mwa Urusi kukutana na Vladimir Putin huko Saint Petersburg siku ya Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.