Pata taarifa kuu

Afrika Kusini, kitovu cha ufadhili wa jihadi?

Afrika Kusini haijawahi kuathiriwa na mashambulizi ya wanajihadi. Demokrasia yake ni imara, uchumi wake ni imara. Hata hivyo, inachukuliwa kuwa ngome ya ufadhili wa kundi la Islamic State (IS) na makundi mengine ya wanamgambo wa Kiislamu.

Wanajeshi wa jeshi la Afrika Kusini wakilinda umati wa watu huko Vosloorus, mashariki mwa Johannesburg, Julai 14, 2021.
Wanajeshi wa jeshi la Afrika Kusini wakilinda umati wa watu huko Vosloorus, mashariki mwa Johannesburg, Julai 14, 2021. AP - Themba Hadebe
Matangazo ya kibiashara

 

Afrika Kusini, nchi iliyoendelea zaidi barani inanyooshewa kidole kwanza na Marekani, ambayo mnamo 2022 ilichukuliwa vikwazo kampuni za Afrika Kusini na raia wanaoshukiwa kuwezesha uhamishaji wa fedha kwa faida ya ISIS, ambapo Afrika imekuwa eneo kuu la kuendesha shughuli zake tangu kupoteza ukhalifa wake kati ya Iraq na Syria mwaka 2019.

"Uangalifu haukutosha kwa miaka 20 kwa sababu Afrika Kusini haikuathiriwa hata kidogo na matatizo ya ugaidi," Hans-Jakob Schindler, mkurugenzi wa kituo cha kutafakari cha Counter-Extremism Project (CEP), ameliambia shirika la habari la  AFP. "Wamarekani ndio walisema: kuna kitu kibaya katika nchi yako," ameongeza mtaalamu huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa. "Serikali nzima sasa iko kazini."

Mnamo mwezi Machi, kikosi Kazi cha Kifedha (FATF), shirika la kupambana na utakatishaji fedha huko Paris, liliweka Afrika Kusini kwenye "orodha ya kijivu" ya nchi ambazo hazina ukali katika vita dhidi ya ufadhili wa shughuli haramu.

"Sasa inakubalika kimataifa kuwa sisi ni kitovu," anasikitika mtaalamu wa kukabiliana na ugaidi kutoka Afrika Kusini Jasmine Opperman. "Afrika Kusini ni uwanja wa kuwinda utumaji pesa (...) mikononi mwa ugaidi", amebaini, pia akimaanisha jukumu la wanaharakati wanaopendelea Al-Qaeda, Hamas ya Palestina au Hezbollah iliyo karibu na Iran.

Martin Ewi, mratibu wa kituo cha uchunguzi wa uhalifu cha Taasisi ya Mafunzo ya Usalama (ISS) huko Pretoria, anathibitisha kwamba "matukio kadhaa yametoa hisia kwamba Afrika Kusini ilikuwa kitovu cha ufadhili wa ugaidi".

Kuongezeka kwa fedha

Jambo linalohusishwa hasa na hali ya kidemokrasia ya nchi na mfumo wa benki ambao umeendelezwa sana na wazi vya kutosha kuruhusu kila aina ya shughuli zilizofichwa. Ufahamu huo unakuja wakati IS, kama Al-Qaeda, imeifanya Afrika kuwa mhimili mkuu wa maendeleo yake. Makundi ambayo yameahidi kutii IS sasa yanaenea nchini Somalia na Sahel, karibu na Ziwa Chad na Msumbiji, na pia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kwa miaka mitano, Afrika imekuwa muhimu zaidi na zaidi" kwa kundi hilo, anabainisha Hans-Jakob Schindler. Lakini jukumu la Afrika Kusini katika kuenea kwa IS lilianza zaidi ya muongo mmoja, anahakikishia Ryan Cummings, mchambuzi wa shirika la kutoa nasaha, Signal Risk, huko Cap.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.