Pata taarifa kuu

Ukraine yakabiliwa na mashambulio wakati huu viongozi wa Afrika wakizuru Kyiv

NAIROBI – Marais wanne kutoka barani Afrika wameanza ziara nchini Ukraine na Urusi kuwasilisha ujumbe wa amani, unaolenga kusitisha mapigano yanayoendelea. Ujio wa marais hao wakiongozwa na Cyril Ramaphosa, umeshudia mashambulio jijini Kyiv nchini Ukraine.

Ujumbe wa viongozi wa Afrika unazuru Kyiv na Urusi kujaribu kupata muafaka wa amani
Ujumbe wa viongozi wa Afrika unazuru Kyiv na Urusi kujaribu kupata muafaka wa amani AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo wa marais wa Afrika, jioni hii unakutana na rais Volodymyr Zelenskyy jioni hii ambapo watawasilisha mapendekezo kutoka barani Afrika kuhusu namna ya kutisitisha vita vinavyoendelea.

Baada ya kuwasili jijini Kiev leo asubuhi kwa usafiri wa treni wakitokea nchini Poland, rais Ramaphosa, na wenzake Macky Sall  Kutoka Senegal, rais wa  Zambia Hakainde Hichilema, na Azali Assoumani wa Comoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, walitembelea mji wa Bucha ambao kuna kaburi la pamoja, walikozikwa watu zaidi ya 400 waliouawa katika   mashambulio ya wanajeshi wa Urusi mwaka uliopita.

Kesho, marais hao wa Afrika watakuwa jijini Saint Petersburg kuona ana raus Vladimir Putin, kumapa mapendekezo hayo ya amani. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa ras Ramaphosa kukutana na raus Putin, baada ya Marekani kudai kuwa Pretoria iiilipa silaha Moscow madai ambayo Afrika Kusini imekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.