Pata taarifa kuu

Afrika Kusini iko tayari kuandaa mazungumzo kati ya Moscow na Kyiv

Afrika Kusini siku ya Alhamisi imetangaza kuwa iko tayari kuandaa mazungumzo ya amani ili kutatua mzozo kati ya Urusi na Ukraine, huku Pretoria mwezi uliopita ikitangaza upatanishi ujao utakaoongozwa na viongozi sita wa nchi za Kiafrika huko Kyiv na Moscow.

Rais Cyril Ramaphosa alikuwa tayari ameeleza mwezi uliopita kwamba viongozi wenzake wa Urusi na Ukraine wote wamekubali kupokea ujumbe wa amani kutoka Afrika.
Rais Cyril Ramaphosa alikuwa tayari ameeleza mwezi uliopita kwamba viongozi wenzake wa Urusi na Ukraine wote wamekubali kupokea ujumbe wa amani kutoka Afrika. © REUTERS / POOL
Matangazo ya kibiashara

"Lazima tuwe wazi kwa uwezekano wa Afrika Kusini kuandaa mkutano wa amani hapa," Waziri wa Ofisi ya Rais Khumbudzo Ntshavheni amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria baada ya mkutano wa baraza la mawaziri.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika mwezi uliopita ilitangaza upatanishi nchini Urusi na Ukraine ili "kupata suluhu la amani" la vita. Misheni inapaswa kuanza katika wiki chache zijazo. Mbali na Pretoria, ujumbe huo unajumuisha wakuu wa nchi za Congo-Brazzaville, Misri, Senegal, Uganda na Zambia.

Ofisi ya Rais Cyril Ramaphosa imesema katika taarifa siku ya Alhamisi kwamba rais wa Afrika Kusini alizungumza kwa simu na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, baada ya "kukaribisha mpango wa wakuu wa nchi za Afrika".

Bw. Ramaphosa alikuwa tayari ameeleza mwezi uliopita kwamba Rais wa Urusi na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, wote wametoa makubaliano yao ya kupokea ujumbe wa amani wa Afrika.

Afrika Kusini, ambayo imekataa kulaani Urusi tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, ikidai kuendelea na msimamo wake wa "kutoegemea upande wowote" na kupendelea mazungumzo, inakosolewa kimataifa kwa ukaribu wake na Moscow. Pretoria imekuwa karibu na Kremlin tangu siku za mapambano ya ubaguzi wa rangi.

Afrika inakabiliwa na ongezeko la bei ya nafaka na matokeo ya vita kati ya Urusi na Ukraine katika biashara ya dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.