Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Ukraine wameripotiwa kusonga mbele katika mji wa Bakhmut

NAIROBI – Nchini Ukraine, wanajeshi wanaripotiwa kusonga mbele kwa lengo la kuwaondoa wanajeshi wa Urusi kwenye mji wa Bakhmut wakati huu Shirika la Msalaba mwekundu likionya kuwa kuharibiwa kwa bwawa kubwa la Kakhovka, litakuwa na madhara makubwa.

Wanajeshi wa Ukraine wameripotiwa kusonga mbele katika uwanja wa mapambano katika mji wa Bakhmut
Wanajeshi wa Ukraine wameripotiwa kusonga mbele katika uwanja wa mapambano katika mji wa Bakhmut AP - Libkos
Matangazo ya kibiashara

Shirika la msalaba mwenkundu linasema kutokana na eneo hilo kujaa maji itakuwa ni vigumu kubaini vilipuzi vilitegwa ardhini.

Maelfu ya watu wamehamishiwa katika maeneo mengine kutoka jimbo la kherson baada ya janga hilo, ambalo Ukraine na Urusi zinalaumiana.

Maeneo mengi ya makazi nchini Ukraine yamefurika maji baada ya kuharibiwa kwa bwawa kubwa la maji
Maeneo mengi ya makazi nchini Ukraine yamefurika maji baada ya kuharibiwa kwa bwawa kubwa la maji AP - LIBKOS

Rais wa Ukraine VolodymyrΒ Zelensky, amesema anashtushwa na hatua ya Umoja wa Mataifa na Msalaba mwenkundu, mashirika anayosema yameshindwa kutoa msaada wa kibinadamu kwa waathiriwa.

Zelesky amesema anasikitika kuwa, baada ya kupita saa nyingi baada ya tukio hilo, hakuna msaada wowote uliotolewa kwa raia wake.

Naye rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema nchi yake inatuma misaada ya kibinadamu nchini Ukraine, baada ya mazungumzo ya njia ya simu na rais Zelensky.

Aidha, amemshtumu kitendo cha kuharibiwa kwa bwawa hilo, kitendo anachosema kinatishia maisha ya wananchi wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.