Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Vita nchini Ukraine: Joe Biden kuthibitisha tena 'msaada wake usioyumba' kwa NATO

Baada ya hotuba yake siku ya Jumanne, rais wa Marekani anatarajia kukutana na viongozi wa nchi tisa za mashariki mwa muungano wa Atlantic

Rais wa Marekani Joe Biden mnamo Februari 21, 2023 huko Warsaw.
Rais wa Marekani Joe Biden mnamo Februari 21, 2023 huko Warsaw. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Joe Biden inakamilika. Rais wa Marekani anakutana Jumatano huko Warsaw na kundi la viongozi tisa wa nchi za NATO za kati na mashariki mwa Ulaya, mbele ya katibu mkuu wa Umoja wa Atlantic, ili kuwahakikishia uungaji mkono "usiotetereka" wa Washington dhidi ya Moscow, siku moja baada ya hotuba ya kivita ya Vladimir Putin, mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita nchini Ukraine.

Joe Biden "atakutana na viongozi wa Bucharest Nine (B9), kundi la washirika wa NATO kwenye upande wetu wa mashariki, mbele ya Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ili kuthibitisha uungaji mkono usioyumba wa Marekani kwa usalama wa Muungano huo," Ikulu ya Marekani imesema katika taarifa yake.

Tangazo hili lauungaji mkono, lililopangwa kutolewa katika ikulu ya rais huko Warsaw, ylinalenga kuzihakikishia nchi hizi tisa (Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Estonia, Hungary, Latvia, Lithuania, Poland, Romania na Slovakia) ambazo zinadaiwa kuwa ni wanachama wa zamani wa Umoja wa Kisovieti au Mkataba wa Warsaw na kuwa kwenye ubavu wa mashariki wa NATO.

Msimamo wa Marekani unakuja siku moja baada ya hotuba kali ya rais wa Urusi, ambaye ameapa kuendeleza mashambulizi yake aliyoanzisha karibu mwaka mmoja uliopita nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.