Pata taarifa kuu

Putin aishtumu Marekani na mataifa ya Magharibi kwa kuchochea vita Ukraine

NAIROBI – Rais wa Urusi Vladimir Putin, ameishtumu Marekani na mataifa ya Magharibi kwa kuchochea vita nchini Ukraine, na kutangaza kuwa nchi yake itasimamisha mkataba wake na Washington kuhusu udhibiti wa matumizi ya silaha za nyuklia.

Rais wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Urusi Vladmir Putin AP - Dmitry Astakhov
Matangazo ya kibiashara

Putin ametoa kauli hiyo akizungumza na viongozi wa kisiasa na kijeshi kwa muda wa saa mbili, kuelekea  siku ya Ijumaa ambayo itakuwa mwaka mmoja, tangu nchi yake ilipoivamia Ukraine kijeshi.

Akionekana mwenye hasira, Putin ameongeza kuwa jeshi la nchi yake, alilolisifu, litaendelea na uvamizi nchini Ukraine na kuongeza kuwa ililazimishwa kuivamia jirani yake.

Pamoja na hilo, amesema vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi yake iliwekewa na mataifa ya Magharibi, havijafanikiwa kuiyumbisha Urusi.

Aidha, amesisisitiza kuwa lengo la Marekani na washirika wake ni kuichochea dunia dhidi ya Urusi na kuwagawa raia wa nchi hiyo, jaribu ambalo amesema halitofanikiwa.

Hotuba hii imekuja siku moja, baada ya rais wa Marekani Joe Biden kufanya ziara ya kushtukiza jijini Kiev na kutangaza msaada zaidi kwa Ukraine na leo yupo nchini Poland kwa mashauriano na viongozi wa jeshi la NATO.

Akijibu hotuba ya Putin, Jake Sullivan mshauri wa masuala ya usalama katika Ikulu ya Marekani, amesema madai ya serikami ya Moscow dhidi ya Washington na washirika wake ni, ni ya kuchekesha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.